April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Sumaye arudi CCM

Spread the love

FREDERICK Sumaye, Waziri Mkuu wa zamani amerejea katika Chama Cha Mapinduzi (CCM), leo tarehe 10 Februari 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Sumaye ametangaza kurejea akiwa kwenye ofisi ndogo ya chama hicho Mtaa wa Lumumba, jijini Dar es Salaam ambapo amepokewa na Dk Bashiru Ally, katibu mkuu wa chama hicho.

Sumaye aliyehuduma kama Waziri Mkuu kwa miaka 10 katika serikali ya Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, ametangaza kurejea CCM kwenye kikao cha ndani cha chama hicho kilichokuwa kikiendelea leo.

Hatua ya Sumaye kuhamia CCM imetanguliwa na kujivua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), zaidi ya miezi miwili iliyopita.

Alijivua uanachama Chadema kwa kile alichokiita ‘figisu’ kwenye uchaguzi wa Uenyekiti wa Kanda ya Pwani Chadema, ambapo licha ya kuwa mgombea pekee, lakini alipigiwa kura nyingi za hapana.

Tarehe 22 Agosti 2015, Sumaye alijiengua CCM na kuhamia Chadema.

error: Content is protected !!