November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

ACT-Wazalendo ‘yawapiga stop’ wabunge wake kwenda bungeni

Spread the love

KIONGOZI wa chama cha upinzani nchini Tanzania, ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe amesema, wananchi wasitegemee kuwaona wabunge wa chama hicho wakienda bungeni. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea)

Zitto amesema, chama hicho kwa sasa hakiwazi suala la ruzuku au wabunge wa viti maalum na kimejikita kufuatilia wananchi na viongozi wao waliojeruhiwa na kushikiliwa kutokana na vurugu za Uchaguzi Mluu wa tarehe 28 Oktoba 2020.

Katika uchaguzi huo, kati ya majimbo 264, ACT-Wazalendo imejipatia majimbo matatu ya Pemba-Zanzibar.

Zitto amesema hayo leo Jumapili tarehe 8 Novemba 202 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisi za chama hicho, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Amesema, zaidi ya wanachama 169 nchi nzima “wamekamatwa katika siku ambazo zimepita na bado wanaendelea kukamatwa, mwenyekiti wetu (Maalim Seif Sharif Hamad) alikamatwa na mimi mwenyewe nilikamatwa na tunaendelea kuripoti polisi.”

Kiongozi huyo amesema, Nasaor Mazrui, naibu katibu mkuu wa chama hicho (Zanzibar) pamoja na wenzake walikamatwa huku Mazrui akipigwa na kumfanya kupoteza fahamu na “polisi walikiri wanaye na mimi mwenyewe juzi Ijumaa nimekwenda ofisi ya DCI nikazungumza na naibu wake akatuthibitishia wanaye Mazrui pamoja na wengine nane.”

Zitto aliyekuwa mgombea ubunge Kigoma Mjini amesema “Ismail Jusa jana amefanyiwa upasuaji wa bega nchini Nairobi-Kenya uliochukua saa saba pamoja na mguu wake uliokuwa umevunjika baada ya kupigwa alipokamatwa. Upasuaji ulimalizika salama.”

Kutokana na hyo, Zitto amesema “kwetu sisi hapakuwa na uchaguzi na kuna taratibu zinaendelea kufanywa ndani ya chama kwa wale waliotangazwa kushindwa, lakini msitegemee kuona wabunge na madiwani waliotokana na ACT-Wazalendo bungeni.”

“Hakuna jambo ambalo ni muhimu zaidi ya uhai wa watu, kiongozi mwenzangu (Mazrui) sijui anaendeleaje, sasahivi siwazi ruzuku, viti maalum wala chochote, nachowaza ni damu ya wanachama wangu na uhai wa viongozi wangu,” amesema.

error: Content is protected !!