September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Mwinyi ateua makamu wa pili wa Rais

Spread the love

RAIS na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amemteua Hemed Suleiman Abdallah kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar …(endelea).

Taarifa ya uteuzi huo wa Abdallah, imetolewa leo Jumapili tarehe 8 Novemba 2020 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Dk. Abdulihamid Mzee.

Abdallah ameteuliwa kushika wadhifa huo ikiwa ni siku moja imepita tangu Rais Mwinyi alipoteua Wajumbe wanne wa Baraza la Wawakilishi akiwemo yeye (Abdallah).

Kabla ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, Abdallah alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Wengine walioteuliwa jana Jumamosi ni; Saada Mkuya Salum ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika utawala wa awamu ya nne chini ya Rais mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete.

Pia wamo; Tabia Maulid Mwita na Juma Ali Khatib.

Abdallah anashika wadhifa huo ambao kwa Tanzania Bara, unaufananisha na waziri mkuu.

Katika utawala uliopita wa Rais mstaafu, Dk. Ali Mohamed Shein, nafasi hiyo ilishikwa Balozi Seif Ali Idd.

Balozi Idd, amehudumu nafasi hiyo kwa miaka kumi mfululizo ya utawala wa Dk. Shein kati ya mwaka 2010 hadi 2020.

error: Content is protected !!