KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameitaka Serikali itoe ratiba ya utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi cha Rais Samia Suluhu Hassan dhidi ya marekebisho ya mfumo wa demokrasia ya vyama vya vingi, akidai kuna juhudi za kuchelewesha mageuzi yake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo, ametoa wito huo leo Alhamisi, tarehe 24 Novemba 2022,akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, ikiwa imepita mwezi mmoja tangu kikosi kazi hicho kikabidhi ripoti yake kwa Rais Samia.
“Tunaitaka Serikali iweke ratiba ya utekelezaji wa mapendekezo ya kikosi kazi ili tuweke mazingira mazuri ya siasa ya nchi yetu tuondoe manung’uniko ya wananchi katika mfumo mzima wa siasa ya nchi yetu, ili Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025 zifanyike kwenye mazingira huru,” amesema Zitto.
Mwanasiasa huyo amesema “tuna wasiwasi kwamba kuna juhudi za kuchelewesha mageuzi haya ili tufike kwenye uchaguzi kukiwa na mazingira yale yale tuliyokuwa nayo 2019 na 2020. Mazingira ya watu kukatwa na kuenguliwa kwenye uteuzi, kugeuza shughuli ya uchaguzi kuwa shughuli ya kipolisi. Tunaona dalili hizo sababu hatuoni shughuli zikifanyika.”
Aidha, Zitto ameishauri Serikali iondoe malalamiko na manung’uniko ya baadhi ya wananchi hususan wanachama wa vyama vya siasa vya upinzani, wanaodai kufanyiwa vitisho na baadhi ya viongozi wa Serikali.
Leave a comment