November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia: TLS ilikuwa chama cha wanaharakati

Rais Samia Suluhu Hassan

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema miaka ya nyuma chama cha Sheria Tanganyika (TLS) kilikuwa si chama cha wanasheria bali wanaharakati kilichokuwa kinapambana na Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Amesema licha ya umuhimu mkubwa wa kufanya kazi na vyama hivyo vya sheria lakini lazima vioneshe kuunga mkono Serikali na kutetea maslahi ya nchi.

“Serikali hatuwashirikishi sana ukiacha wale wa Serikali ninyi hatuwashirikishi, lakini kila decision zinazofanywa ni rationaly, sasa angalie kulikuwa na sababu gani ya kutowashirikisha,” amesema Rais Samia na kuongeza;

“Lakini embu tuangalie mfano Tanzania miaka michache iliyopita tulikuwa na chama cha Tanganyika Law Society ambacho kiliwa si chama cha wanasheria bali chama cha wanaharakati na mapambano yao ilikuwa dhidi ya Serikali.

“Sasa mimi nikijua wewe ni dhidi yangu tutashirikishana? siwezi kukushirikisha lazima unioneshe Am here to support you, Am here to serve the country nikiona una sura hiyo nitakushirikisha na nikiona una sura ya uadui nami sitoweza kukushirikisha, utatumia sheria zote za kimataifa zote na mimi ntatumia zangu kukuvaa usishiriki kwangu.”

Rais Samia amesema amefurahishwa nimefurahi kusikia kuwa Chama cha Sheria Afrika Mashariki ambacho kinajumuisha vyama vya kila taifa, vinataka kushir,iana na Serikali.

“Nilivyosikia haya ya leo nikasema this people are now coming to their sense, nimefurahi kuyasikia niliyoyasikia,” amesema.

error: Content is protected !!