October 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Zitto akwama, mahakama yakwama

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo tarehe 7 Oktoba 2019, imekwama kuendelea na kesi ya uchochezi inayomkabili Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini kwa madai ya kufiwa. Anaripoti Faki Sosi…(endelea).

Peter Kibatala, Wakili wa Utetezi amemweleza Hakimu Mkazi mkuu, Huruma Shaidi kwamba mteja wake (Zitto), amefiwa mkoani Kigoma hivyo ameshindwa kufika mahakamani hapo.

Kesi hiyo ilikuwa imefika mbele ya Hakimu Huruma kwa ajili ya kusikilizwa. Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo anakabiliwa na kesi ya uchochezi, anadai wa kutenda makossa hayo tarehe 28 Oktoba 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam.

Nassoro Katuga, wakili wa serikali mbele ya Hakimu Shaidi alisema, shauri hilo lilikuwa limefikishwa kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa ambapo tayari mashahidi wane wametoa ushahidi wao.

Hakimu Huruma amepanga kuendelea kusikiza shuri hilo tarehe 22, 23 Oktoba 2019.

error: Content is protected !!