Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema kwatibuka, Mbowe aambiwa ‘inatosha’
Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwatibuka, Mbowe aambiwa ‘inatosha’

Spread the love
JOTO la uchaguzi wa viongozi ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), tayari Cecil Mwambe ambaye ni Mbunge wa Ndanda ameanza kumtingisha Freeman Mbowe kwenye nafasi ya uenyekiti wa chama hicho taifa. Anaripoti Faki Sosi…(enedelea).

Mwambe amemtaka Mbowe kuachia ngazi, na kwamba wakati umefika kuwaachia wengine nafasi hiyo ya uenyekiti, baada ya kuishikilia kwa muda mrefu.

Akizungumza na chombo kimoja cha habari, Mwambe amemshukuru Mbowe kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika chama hicho katika kipindi chote cha uongozi wake.

“Tunamshukuru kwa mchango wake alioutoa katika chama chetu, lakini nadhani umefika wakati wa kuwaachia kiti wengine,” amesema Mwambe.

Kauli hiyo ya Mwambe imekuja siku sita kadhaa baada ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kukipa chama hicho siku saba, kutoa maelezo kwa nini kilisichukuliwa hatua kwa kukawia kufanya mkutano mkuu na uchaguzi wa viongozi wake wa kitaifa.

Dk. Vincent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema, amesema wanatarajia kufanya uchaguzi tarehe 18 Desemba 2019. Mbowe ameongoza chama hicho katika nafasi ya uenyekiti kwa miaka 15.

Cecil anakuwa mwanachama wa kwanza kwenye uchaguzi huu kutangaza kutaka nafasi ya uenyekiti zikiwa zimebaki siku 11 kuingia kwenye uchaguzi huo.

Mbowe alianza kuongoza chama hicho mwaka 2004 kutoka kwa aliyekuwa mwenyekiti wake Bob Makani. Makani alifariki dunia tarehe 10 Juni 2012.

Nafasi ya uenyekti wa Mbowe ulipaswa kukoma tarehe 14 Septemba 2019, ambapo Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imekiandikia barua chama hicho kieleze sababu za kuchelewa kufanya uchaguzi wa viongozi kwa mujibu wa Katiba yao.

Ndani ya Chadema, kampeni za kutaka Mbowe aendelee kuwa mwenyekiti wa chama hicho zimekuwa zikifanywa mkoa kwa mkoa. Hata hivyo, ndani ya chama hicho wapo wanaotaka uongozi wa Mbowe ufike tamati kwenye uchaguzi wa mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

error: Content is protected !!