Saturday , 3 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto aibuka na mbinu ya kuing’oa CCM
Habari za SiasaTangulizi

Zitto aibuka na mbinu ya kuing’oa CCM

Spread the love

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe aeleza mbinu zitakazotumiwa na chama hicho kukiondoa madarakani  Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia uchaguzi wa serikali za mitaa na  uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Halmashauri kuu ya chama hicho leo tarehe 29, Septemba 2019, amesema kuwa Serikali ya CCM kwa kipindi cha miaka minne hakikukidhi matakwa ya wananchi hususani katika  uchumi.

“Uchaguzi wowote huhusu mambo ambayo yapo juu …unahusu mambo ambayo yapo chini wao wakija juu na ndege zao nyie nendeni chini na njaa za wananchi ambayo imesababishwa na sera za CCM.

“Wakija juu na Reli zao nyie nende chini na hali ya elimu katika maeneo yao wakija juu na ‘stieglers gorge’ nyie nendeni chini kuangalia maelfu ya vijana ambao hawana ajira wanateseka wakija juu la lolote lao nyie angalie yanayowagusa wanachi moja kwa moja,” amesema Zitto.

 Amesema kuwa ni watanzania wachache wanaoamini katika maendeleo ya vitu baadala ya watu kwa kuwa watu hawawezi kufanya shughuli za uchumi.

“Ni asilimia tano pekee ya  Watanzania wanaopanda ndege acheni wapigiwe kura na hiyo asilimia tano …hata hiyo tano hawatakuwa nayo yote mimi napanda ndege na sitawapigia kura,” anesema Zitto.

Amewataka wanachama wa chama hiko kuwaendea wananchi na kuwapigania juu ya masuala yanayogusa maisha yao moja kwa moja ndipo watakapoeleweka.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

error: Content is protected !!