Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Butiku: Tuko kwenye wakati mgumu
Habari za SiasaTangulizi

Butiku: Tuko kwenye wakati mgumu

Spread the love

MZEE Joseph Butiku, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, amevitaka vyama vya siasa kufuata misingi ya Katiba, ili kuirudisha nchi kwenye mstari ulionyooka. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza katika uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya Asasi za Kiraia ya mwaka 2019/2020,uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mzee Butiku amesema Taifa limetetereka katika kutumia katiba na sheria.

“Tulitetereka kidogo kwenye kutumia katiba na sheria, na ndio maana tulipojitahidi kurekebishika ilikua ngumu. Sasa kurudi si rahisi,” amesema Mzee Butiku.

Mzee Butiku ameeleza kuwa, vyama vya siasa vinatakiwa vitambue ya kwamba Tanzania si mali yao, bali ni mali ya Watanzania.

“Vyama vitambue kwa mujibu wa katiba, Tanzania sio yao, ni ya Watanzania na wako kwa ajili ya kusimamia shughuli za Watanzania. Viongozi wa ndani ya vyama watambue hivyo hivyo,” amesema Mzee Butiku na kuongeza;

“Na wafanye jitihada za kulielewa hili zaidi. Na itakapohitajika kufanya mabadiliko, ifanye kwa utaratibu. Serikali ya sasa hivi ni ya CCM, tunaisema. Lakini kwa serikali zijazo utaratibu ni huo huo, tutasema kwani ndivyo tulivyokubaliana.”

Mzee Butiku amesema ni vyema serikali, vyama vya siasa, asasi za kiraia na Watanzania kwa ujumla wakatambua kwamba kila mtu ana wajibu wa kuheshimu uhuru, utu na haki za binadamu.

“Tunastahili haki za binadamu kama zinavyotajwa kwenye katiba. Kwa nini tunabishana? Wengine waoga, hamuwezi kusema, wengine ni wanafiki hawawezi kusema,” amesema Mzee Butiku.

Ameeleza kuwa, Taifa lililojaa waoga, wanafiki na wapenda fedha haliwezi kusimamia na kujenga haki.

“Mimi nikiwa rais,  mshauri wangu akiwa muoga, atanisaidia? Nimewahi kuwa msaidizi wa rais, ni kazi ngumu. Huwezi kumsaidia kama muoga, mnafiki, mzurulaji, mwizi na mpenda hela, huwezi,” amesema Mzee Butiku.

Mzee Butiku amesema ni jukumu la kila Mtanzania, kuisimamia serikali kwa kuwa bila wananchi hakuna serikali.

Amesema hata Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alichukia watu wanafiki, na kwamba alitaka watu wazungumze.

“Baba wa Taifa alituachia utamaduni wa kuzungumza, hakuogopa wazungumzaji. Kikubwa kwake ni mazungumzo, majadiliano. Alichukia tabia ya watu kujitutumua na kuonea watu. Alitaka watu wazungumze,” amesema Mzee Butiku.

Wakati huo huo, Mzee Butiku amekemea tabia ya baadhi ya vijana kufanya siasa chafu kwa kuwatukana watu, na kutoa wito kwa wazee kuwakanya vijana wenye hulka hizo.

“Vijana msiwe makuwadi, acheni kuwa makuadi. Mnatumwa kutukana, muache na nyie wazee mkiwaona muwaite muwaseme. Hatuwezi, wakati tuna vikao, tuna vyama. Watoto wanatok, wanatukana hivi hivi, hii ni tabia gani  taifa gani?” amehoji Mzee Butiku na kuongeza;

“Watu wenye tabia hii ni uhuni, haifai haifai haifai.Tumsaidie rais wetu. Wakati mwingine unaweza ukadhani anatumwa, anatumwa na nani

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Chadema yamtaka Rais Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!