Wednesday , 27 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Watuhumiwa 467 uhujumu uchumi waomba toba, kulipa Bil. 107.1
Habari za SiasaTangulizi

Watuhumiwa 467 uhujumu uchumi waomba toba, kulipa Bil. 107.1

Biswalo Mganga, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP)
Spread the love

WATUHUMIWA 467 wa uhujumu wameomba toba, na kukubali kurejesha serikalini fedha walizotafuna zaidi ya Sh. 107.1 bilioni. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Hayo amesema Biswalo Mganga, Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), leo tarehe 30 Septemba 2019, Ikulu Jijini Dar es Salaam, wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa Rais John Magufuli hivi karibuni, wa kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali.

DPP Mganga ameeleza kuwa, baadhi ya washtakiwa hao wako tayari kulipa Sh. 13.6 bilioni muda wowote kuanzia sasa, wakati wengine wameomba kulipa kwa awamu kiasi cha Sh. 94.2 bilioni.

“Katika kundi hilo, watu ambao wako tayari kurudisha moja kwa moja fedha jumla ni  Sh. 13.6 bilioni,” amesema DPP Mganga na kuongeza.

“Kundi la pili wako tayari kulipa kwa awamu, jumla yake Sh.  94.2 bilioni. Wako tayari kurudisha, wanasema watalipa kidogo kidogo. Ukijumlisha zote kwa wasthakiwa 467,  jumla ya fedha washtakiwa wa hujumu wako tayari kurudisha ni Sh.  107.1 bilioni.”

Hata hivyo, DPP Mganga amesema kuna baadhi ya watuhumiwa walishafuata taratibu za kisheria na kulipa mahakamani zaidi ya Sh. 1.40 bilioni, siku ya Ijumaa iliyopita.

“Ijumaa iliyopita kuna mtu mmoja alikubali kuitikia wito, alikiri mahakamani. Alikuwa andaiwa dola laki 4.5 alikubali kulipa pale pale. Thamani yake ni Sh. 1.3 bilioni, bado alilipishwa faini ya Sh. 5 milioni mahakamani.

“Ijumaa hiyo hiyo, kuna mtu alikuwa na gram 2123.64 za madini ya vito, yenye thamani ya Sh. 36.5 milioni, huyu alikiri na akalipa hizo fedha na madini hayo yakataifishwa,” amesema DPP Mganga.

Tarehe 22 Septemba 2019, Rais Magufuli alitoa mapendekezo kwa DPP Mganga, ya kutoa msamaha kwa watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kuomba toba na kurejesha fedha au mali walizofisadi, ndani ya siku saba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!