Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto afungua kesi kupinga muswada, yahairishwa mpaka mchana
Habari za SiasaTangulizi

Zitto afungua kesi kupinga muswada, yahairishwa mpaka mchana

Spread the love

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe na wenzake wawili, Joran Bashange na Salim Bimani wamefungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa imehairishwa hadi leo saa nane mchana. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Kesi hiyo imefunguliwa leo katika Mahakama Kuu dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupingaMuswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa na kuzuia usijadiliwe bungeni mpaka kesi ya msingi itakaposikilizwa.

Kwa mujibu wa Ado Shaibu, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi, ACT Wazalendo, kesi hiyo imehairishwa mpaka saa nane ambapo Mahakama Kuu itaamua kuhusu hoja kuu mbili zilizozua ubishani mkubwa wa hoja baina ya upande wa wanasheria wa waombaji (Applicants) na upande wa Mwanasheria Mkuu wa serikali.

Hoja zilizoibua mvutano ni upande wa muda wa Mwanasheria Mkuu wa serikali kujibu hoja zilizoibuliwa na waombaji uongezwe kama ilivyoombwa na upande wa AG au upunguzwe kama ilivyoombwa na upande wa waombaji.

Pia kama Mahakama iweke zuio (Injunction) la kuzuia muswada kujadiliwa Bungeni, kama ilivyoombwa na waombaji mpaka kesi ya msingi itaposikilizwa na kuamuliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!