Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Safari aongoza jopo la mawakili kuikoa Chadema
Habari za SiasaTangulizi

Prof. Safari aongoza jopo la mawakili kuikoa Chadema

Spread the love

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tanzania Bara, Prof. Abdallah Safari, sasa atakuwa amejitosa rasmi kuokoa chama chake. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Prof. Safari ambaye ni wakili wa mahakama kuu, leo Alhamisi, tarehe 3 Januari 2018, ameungana na jopo la mawakili saba wa Chadema, kuwatetea viongozi wakuu wa chama hicho.

Viongozi hao wakuu wa Chadema, wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, wanakabiliwa na kesi ya jinai kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Mbowe na mshitakiwa mwingine kwenye kesi hiyo – mbunge wa Tarime Mjini na Mweka Hizina wa Baraza la Wanawake wa Chadema, Esther Matiko – wanashikiliwa katika gereza kuu la Segerea, kufuatia kuwafutiwa dhamana na mahakama.

Washitakiwa wengine kwenye kesi hiyo ya jinai Na. 112/2018, ni pamoja na katibu mkuu wa chama[M1]  hicho, Dk. Vicenti Mashinji; mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa; mbunge wa Kibamba na naibu katibu mkuu Bara, John Mnyika.

Wengine katika kesi hiyo, ni mbunge wa Kawe, Halima Mdee; mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche; mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya na naibu katibu mkuu wa chama hicho, upande wa Zanzibar, Salum Mwalimu.

Mbowe na Matiko, walifutiwa dhamana zao, tarehe 23 Novemba mwaka jana kwa madai kuwa walishindwa kutimiza masharti waliyopewa.

Mawakili wengine kwenye kesi hiyo, ni pamoja na Peter Kibatara, Dk. Rugemeleza Nshalla, Jeremia Mtobyesa, Fredrick Kihwelo na Faraja Msemwa.

Prof. Safari, ni mmoja wa wanasheria mashuhuri katika ukanda huu wa Afrika Mashariki kwenye masuala yanayohusu jinai. Mara kadhaa amesaidia kwenye ushauri wa kisheria majaji wa mahakama ya rufaa, kwa lengo la kurahisisha utoaji wa haki.

Akizungumza mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi wa mahakama ya Kisutu, Wilbrad Mashauri, Prof. Safari alihoji hatua ya upande wa mashitaka kuwasilisha mahakama ya rufaa, maombi ya rufaa kwa njia ya kawaida.

Alisema, “kesi hii imefunguliwa mahakama kuu kwa hati ya dharura. Hivyo basi, tunatarajiwa kuwa upande wa mashitaka utatumia nja hiyo hiyo kuwasilisha rufaa yao mahakama ya Rufaa.”

Akijibu hoja ya Prof. Safari, wakili wa serikali mkuu, Paul Kadushi alisema, upande wa utetezi hauna uhalali wowote wa kisheria wa kutaka kujua au kuhoji jambo hilo.

Hata hivyo, Hakimu Mashauri aliutaka upande wa utetezi kufuatilia suala hilo mahakama ya rufaa. Hakimu Mashauri alighairisha kesi hiyo hadi tarehe 17 Januari mwaka huu.

Mbowe na wenzake wanakabiliwa na jumla ya mashitaka 13, ikiwamo kula njama, kuhamasisha hisia za chuki, uchochezi, kufanya mkusanyiko wenye ghasia na kushawishi wananchi katika hali ya kutoridhika, kufanya vurugu na kuvunja Amani.

Mbele ya mahakama, Mbowe na watuhumiwa wenzake, wanadaiwa kuwa kati ya Februari 1 na 16 mwaka jana, katika maeneo ya Dar es Salaam, walipanga njama za kufanya ghasia, kuandamana na kusababishia mauaji, mwanafunzi wa mwaka wa pili wa chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT), Akwiline Akwilina.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!