Friday , 9 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Ziara ya Rais Magufuli yawaibua Chadema
Habari za SiasaTangulizi

Ziara ya Rais Magufuli yawaibua Chadema

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimepinga kauli za Rais John Magufuli alizozitoa alipokuwa kwenye ziara yake Kanda ya Ziwa. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza leo tarehe 12 Septemba 2018 na Waandishi wa Habari, Dk. Vicent Mashinji, Katibu Mkuu wa Chadema ambapo amesema kauli na uendeshaji wa ziara Rais John Magufuli umekuwa hauendani na mipango ya maendeleo nchini.

Amesema Uendashaji wa Ziara ya Rais imekuwa ya kisiasa na siyo ya kiserikali ambayo ilikuwa ikiegemea upande mmoja wa chama chake.

“Rais Magufuli amekuwa akiusikiliza upande mmoja ule unaomuunga mkono na kuwanyamazisha wengine ambao ni viongozi ambapo hawezi kusikia maoni ya upande mwengine ilhali kuwa wangeweza kutoa mchango chanya kwenye maendeleo,” amesema Dk. Mashinji.

Amesema kuwa Chadema kimeona kuwa taasisi ya Urais imekuwa ikinadi ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kwamba amekuwa akiendeleza siasa kila uchwao ilhali amekataa watu wengine wasifanye siasa.

“Ni aibu mtumishi wa umma kumuona ofisini akiwa na ilani ya CCM kwani ni ishara kuwa ofisi ipo kisiasa,” amesema Dk. Mashinji.

Amesema kuwa ziara za Rais John Magufuli zimekuwa zikiwakashifu viongozi wa umma waliotofauti kiitikadi ya chama chake.

Wakati huo huo Mashinji ambaye ni daktari kitaaluma amesema kuwa kauli ya Rais ya kupinga uzazi mpango haina afya ya maendeleo ya taifa kutokana na hali ya uchumi wa nchi.

Amesema kuwa Tanzania imekuwa nchi ambayo ni muhanga wa huduma ya afya hasa kwenye zahanati ambazo hazijaboreshwa na sio rafiki kwa kina Mama kujifungua.

“Wakinamama wengi wamekuwa wakifariki kutoka na ubovu miondominu ya hospitali ambapo kina mama 400 kati ya 100,000 walikiwa wakifariki.

“Miye nimekuwa daktari Muhimbili pale nimeshuhudia namna kina mama wajazito walikuwa wakipata tabu kutokana na uhaba wa wataalamu na wauguzi sambasamba na vifaa tiba na vyumba vya kujifungulia,” amesema Dk. Mashinji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaTangulizi

Ngoma bado mbichi mkataba wa Bandari

Spread the love  SAKATA la mkataba wa uendeshaji, uendelezaji na uboreshaji wa...

BiasharaTangulizi

Mkurugenzi TPA: Mkataba unaweza kuvunjwa

Spread the loveMKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),...

BiasharaTangulizi

Mkurugenzi TPA: Mikataba ya utekelezaji bado haijasainiwa

Spread the loveMKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),...

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

error: Content is protected !!