March 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waliosambaza vitabu feki watimuliwa kazi

Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu

Spread the love

WATUMISHI takribani 29 wa Taasisi ya Elimu nchini (TIE) wamesimamishwa kazi na kufunguliwa mashtaka ya kinidhamu kutokana na sakata la baadhi ya vitabu vya kujifunzia wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu vyenye makosa kutumika shuleni. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Hayo yamesemwa leo tarehe 12 Septemba 2018 jijini Dodoma na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati akijibu swali la Mbunge wa Nanyamba, Abdallah Chikota aliyehoji hatua iliyochukuliwa na serikali kuhusu sakata hilo, katika kipindi cha maswali na majibu.

Sakata hilo liliibuliwa bungeni mwaka jana wakati wabunge wakichangia bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha wa 2017/18, ambapo walisema vitabu hivyo vilikuwa na makosa ya usanifu, picha za vitabu kucheza na makosa ya lugha.

“…Watumishi 29 wamesimamishwa kazi na kufunguliwa mashtaka ya kiinidhamu ambapo yakithibitika watachukuliwa hatua za kinidhamu,” amesema Waziri Ndalichako.

Aidha, Waziri Ndalichako amesema serikali imesambaza huleni vitabu zaidi ya 9,000 vya darasa la kwanza hadi la tatu.

error: Content is protected !!