Tuesday , 27 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yamwinda Maalim Seif, CUF yang’aka
Habari za SiasaTangulizi

Chadema yamwinda Maalim Seif, CUF yang’aka

Spread the love

VITA vya kisiasa ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) vinawasogeza karibu viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na sasa wanampigia hesabu Maalim Seif Sharif Hamad, Katibu Mkuu wa chama hicho. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Chadema imeeleza kuwa, Maalim Seif atakuwa mgombea urasi wake kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 visiwani Zanzibar pale mgogoto wa chama hicho utaposhindwa kupatiwa ufumbuzi na chama hicho kuparaganyika.

Taarifa ya mwanasiasa huyo kuwindwa na Chadema kugombea urais visiwani humo kwenye uchaguzi mkuu ujao imetolewa leo tarehe 11 Septemba 2018 na Hashimu Juma, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Chadema.

Juma mesema kuwa, ndoto ya upinzani ni kushika dola na kwamba, CUF Zanzibar imeimarika kupitia Maalim Seif na kwamba, kwa upande wa Bara Chadema ndio iliyoimarika hivyo kwa umoja wa vyama hivyo viwili, malengo yao yatafikiwa.

Amesema kuwa, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimekuwa kikitumia mbinu chafu za kisaia kwa kuibua migogoro ndani ya vyama vya siasa nchini kama walivyokitibua chama cha CUF ya kukifanya kuwa na vipande viwili ili kisiweze kufanya operesheni yoyote ya kisiasa.

Juma amesema kuwa Chadema itampa nafasi Maalimu Seif ya kugombea nafasi ya urais ndani ya `chadema visiwani Zanzibar na huku wabunge wake wakiwa kwenye nafasi zao kwenye majimbo yao.

Amesema kuwa CUF hakina uwezo wa kusimamisha mgombe kwa sasa kutokana na mgogoro uliopandikizwa ndani ya chama hicho.

Mbarara Maharagande, Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma amesema kuwa, CUF hawana mpango uliotangazwa na chadema kwamba, Maalim Seif anaweza kugombea urais kupitia chama hicho.

“Si mpango wa CUF kuungana na Chadema kama ambavyo imeelezwa na Chadema, CUF itaendelea kusimama yenyewe na tutaendelea kushirikiana kwa mambo mengine kama ilivyo sasa,” amesema Mbarara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!