Wednesday , 1 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Zaidi ya milioni 300 kutolewa msimu wa 4 NMB- ‘MastaBataKotekote’
Habari Mchanganyiko

Zaidi ya milioni 300 kutolewa msimu wa 4 NMB- ‘MastaBataKotekote’

Spread the love

 

KATIKA kuhamasisha wateja wa Benki ya NMB kutumia kadi ‘master card’ pamoja na mfumo wa NMB Mkononi kufanya miamala badala ya kutumia fedha taslimu, benki hiyo inatarajia kutumia zaidi ya Sh milioni 300 kugawa zawadi mbalimbali kupitia promosheni ya ‘Masta Bata Kotekote’.

Hatua hiyo inakuja baada ya NMB kuzindua msimu wa nne wa promosheni hiyo ya ‘Masta Bata Kotekote’ wenye lengo la kuwahamasisha wateja wake kutumia kadi kufanya malipo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Drbes Salaam … (endelea).

Hayo yamebainishwa juzi jijini Dar es Salaam na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard wakati akichezesha droo ya kwanza ya Masta Bata Kotekote msimu wa nne.

Katika droo hiyo, mshindi wa mwanzo alipewa bodaboda huku washindi wengine 75 wakipewa fedha taslim Sh 100,000.

Aidha, Richard alisema droo hiyo itachezeshwa kila wiki ambapo mshindi atapata fedha taslim na wengine kushinda bodaboda.

“Pia kila mwezi mshindi atapata bodaboda mbili na fedha taslimu zitatolewa kwa washindi wengine wakati Grand finale jumla ya washindi saba watapata fursa ya kwenda Dubai na Zanzibar ambapo kila mshindi atakwenda na mwenzake au rafiki katika safari hiyo,” alisema.

Alisema Benki ya NMB imekuwa ikiendelea kuwahamasisha watanzania kupitia kampeni mbalimbali kutumia zaidi kadi kufanya malipo badala ya kutumia fedha taslim ambapo pia kadi hiyo hutumika kufanya malipo ndani na nje ya nchi.

“Mnafahamu kwa muda mrefu tumekuwa na kampeni mbalimbali za kuhakikisha watanzania wanatumia zaidi kadi na tumekuwa tukishirikiana na wenzetu wa Master card kuhakikisha tunaendeleza utamaduni huu wa kuitumia kadi badala ya pesa taslimu.”

“Ukiwa na kadi yako unaweza kuitumia popote ukwia ndani au ukienda nje ya nchi,” amesema Richard.

Ametoa wito kwa watanzania kuendelea kutumia master card kufanya malipo ili kujiweka katika nafasi ya kushinda zawdi hizo za Masta bata kotekote zilizoandaliwa msimu wa nne.

Aidha, Meneja Mwandamizi Idaraya Biashara za Kadi, Manfred Kayala amesema droo hiyo itachezeshwa kwa zaidi ya miezi mitatu na kuwasisitiza wateja kuendelea kutumia zaidi kadi katika kufanya malipo.

“Ili kurudisha faida tuliyoipata kama benki kwa wateja wetu, wiki mbili zilizopita tulizindua promosheni hii pale Mbeya ambapo tutashuhudia zawadi za pesa taslim zaidi ya milioni 350, pikipiki na safari mbalimbali.

“Wateja wetu mnashauriwa kutumia kadi badala ya kutumia pesa taslimu, ambayo tunajua kwamba pesa taslimu kutembea nazo inakuwa ni changamoto, zoezi hili tutakuwa tunalifanya kwa takribani miezi zaidi ya mitatu na washindi nmbalimbali watapatikana,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

Habari Mchanganyiko

TMA yapongezwa kuimarisha ubora na usahihi wa taarifa za Hali ya Hewa

Spread the love  WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA),...

error: Content is protected !!