November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

566,840 kidato cha IV kuanza mitihani ya Taifa kesho

Wanafunzi wakifanya mtihani

Spread the love

WATAHINIWA 566,840 wa kidato cha nne nchini Tanzania wanatarajia kuanza mitihani yao ya Taifa kesho Jumatatu tarehe 14, Novemba, 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar…(endelea).

Idadi hiyo ya watahiniwa inajumuisha  wanafunzi kutoka shule 5,212 na vituo vya watahiniwa wa kujitegemea 1,794.

Hayo yameelezwa leo Jumapili tarehe 13, Novemba, 2022 na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), Athumani Amasi, wakati akizungumzia kukamilika kwa maandalizi ya mitihani hiyo.

Amasi amesema kati ya watahiniwa 566,840 waliosajiliwa kufanya mitihani hiyo, 535,001 ni wa shule, na 31,839 ni wakujitegemea.

Kati ya watahiniwa hao, 247,131 ni wavyulana sawa na asilimia 46.19 na wasicana ni 287,870 sawa na asilimia 53.81 huku wenye mahitaji maalumu wakiwa 852 ya watahiniwa wote.

Kwa mujibu wa Amasi maandalizi yote ya kufanya mitihani hiyo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa mitihani na vijitabu vya kujibia.

Aidha metoa wito kwa kamati za mitihani za mikoa yote kuhakikisha taratibu zote za uendeshaji wa mitihani ya Taifa zinazingatiwa ipasavyo.

error: Content is protected !!