Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Samia, Dk. Mwinyi kukutana na mabalozi 45 wa Tanzania
Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia, Dk. Mwinyi kukutana na mabalozi 45 wa Tanzania

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

 

JUMLA ya mabalozi 45 wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani wanatarajiwa kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Mkutano huo umepangwa kufanyika mjini Zanzibar kuanzia tarehe 14 hadi 21 Novemba 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mkutano huo ambao ni wa kwanza baina ya Rais Samia na Mabalozi tangu Serikali ya Awamu ya Sita kuingia madarakani, umebeba Kaulimbiu ya “Mwelekeo Mpya Katika Kuimarisha Diplomasia ya Uchumi”.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es salaam leo tarehe 12 Novemba, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga wakati akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo, Dk. Stergomena Tax.

Amesema lengo la mkutano huo ni kutoa fursa kwa Mabalozi na watendaji wa Wizara wanaoshiriki katika uratibu wa utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje kupokea maelekezo ya Rais Samia pamoja na viongozi wengine kuhusu mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Sita katika utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi.

Pia unalenga kubadilishana uzoefu katika utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi, kuainisha changamoto katika utekelezaji wa majukumu na kuja na mikakati madhubuti ya namna ya kuzitatua changamoto mbalimbali za kiutendaji, kwa lengo la kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.

Dk. HUssein Mwinyi, Rais wa Zanzibar

Aidha, amesema mkutano huo ni fursa kwa Tanzania kuandaa mikakati ya pamoja ya namna ya kujiweka sawa ili kuhakikisha Taifa linanufaika ipasavyo kutokana na fursa mbalimbali zilizopo katika maeneo ya uwakilishi.

Akifafanua ratiba ya mkutano huo, Balozi Kasiga amesema tarehe 14 Novemba, 2022, Waziri Dk. Tax atafungua kikao cha Mabalozi, Konseli Wakuu na Menejimenti ya Wizara ambacho kitafanyika mpaka tarehe 17 Novemba, 2022.

“Katika siku hizo tumealika wadau mbalimbali wa Sekta ya umma na binafsi kuongea na waheshimiwa Mabalozi masuala mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa majukumu yao.

“Tarehe 17 Novemba, 2022 Mabalozi na Menejimenti ya Wizara watatembelea vivutio vya utalii na miradi ya maendeleo ya kimkakati Zanzibar ikiwa ni pamoja na Bandari ya Malindi na Manga Pwani; Tarehe 18 Novemba, 2022 kutakuwa na Mkutano kati ya Rais Dk. Mwinyi na waheshimiwa Mabalozi na Menejimenti ya Wizara; na tarehe 19 Novemba, 2022 kutakuwa na Mkutano kati ya Rais Samia na Mabalozi na Menejimenti ya Wizara,” amesema.

Aidha, amesema Mabalozi wote kutoka Balozi zote 45 wanaoiwakilisha nchi yetu nje ya nchi watakuwepo nchini na moja ya majukumu waliyoelekezwa ya kufanya ni kujulisha umma kuhusu utekelezaji wa majukumu yao.

Amesema baada ya mkutano huu Balozi hizo zitajipanga upya ili kuongeza ubunifu katika kuiletea nchi maendeleo ili kufikia azma ya Serikali ya Dira ya Maendeleo ya 2025.

“Hadi ninavyoongea na nyinyi, Balozi zimefanya kazi nzuri na ya kuridhisha ya kutafuta wawekezaji, masoko ya bidhaa zetu, misaada na mikopo nafuu ya maendeleo na kuvutia watalii wengi kuja nchini.

“Mfano mzuri wa hivi karibuni ni ziara za viongozi wetu wakuu, Rais Samia nchini China, ziara ya Makamuwa Rais Dk. Philip Mpango nchini Ivory Coast, ziara ya Rais Dk.Mwinyi nchini Oman na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa nchini Jamhuri ya Korea.

“Ziara hizo zimeratibiwa vizuri na Balozi zetu na zimekuwa na mafanikio makubwa katika diplomasia ya Tanzania,” amesema.

 

1 Comment

  • Sera yetu kuhusu masuala ya Palestina yakoje? Je tunawaunga mkono Wapalestina katika juhudi zao za kujikomboa au tunaunga mkono ukoloni na ukandamizaji wa Israel? Naulizaa kwa sababu wasiwasi wangu ni kujali zaidi mikopo na uwekezaji kuliko utu wa mwanadamu kama tulivyofundishwa na Mwalimu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

error: Content is protected !!