August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yamtangaza mrithi wa Muro

Dismas Ten, Afisa Habari wa Yanga (katikati) akizungumza baada ya kutanganzwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa (kulia)

Spread the love

KLABU ya Yanga imemtangaza Dismas Ten kuwa Ofisa habari wa klabu hiyo ambaye anachuku nafasi ya Jerry Muro, anaandika Jovina Patrick.

Dismas ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari, kabla ya uteuzi huo alikuwa Afisa Habari wa timu ya Mbeya City, anachukua nafasi ya Muro aliyekuwa anatumikia kifungo cha mwaka mmoja.

Muro alifungiwa kutojihusisha na habari kwa mwaka mmoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) hivyo kufanya nafasi hiyo kuwa wazi kwa muda wote mpaka Dismas alipoteuliwa.

Charles Mkwasa, Katibu Mkuu wa Yanga amemtangaza Dismas kuwa Ofisa Habari cheo ambacho pia kilipewa jina la Mkurugenzi wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano.

Baada ya utangazwa kushika nafasi hiyo, Dismas amesema anafurahi kupewa nafasi hiyo na anaamini atafanya kazi vizuri kwa kushirikiana na wanahabari kwa kuwa amekuwa akifanya hivyo tangu alipokuwa katika ajira yake iliyopita.

 

error: Content is protected !!