August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Risiti za mafuta kaa ya moto kwa vituo

Christina Mndeme, Mkuu wa Dodoma, akishirikiana na Maofisa ya TRA Dodoma wakifunga moja kati ya vituo nane visivyokuwa na risiti

Spread the love

CHRISTINA Mndeme, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini amevifungia vituo nane vya mafuta visivyofuata sheria za utendaji wilayani hapo ikiwemo kutokuwa na mashine za kutolea risiti, anaandika Irene Emmanuel.

Katika ziara hiyo, Christina Mndeme amekagua utendaji wa vituo hivyo vya mafuta ikiwemo ulipaji kodi na utoaji wa risiti baada ya huduma kwa kufunga mashine za EFD zinazofungwa moja kwa moja kwenye pampu au mita ya mafuta.

Vituo nane kati ya tisa vimefungwa kwenye ziara hiyo kutokana na madai ya kutofuata sheria na utaratibu wa biashara wa utoaji risiti na kubaki kituo kimoja tu kinachofata sheria hizo.

Kazi hiyo ilifanywa kwa ushirikiano wa maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Dodoma mjini.

error: Content is protected !!