May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bunge limepoteza sifa yake-Mngwali

Jengo la Bunge la Tanzania mjini Dodoma

Spread the love

RIZIKI Shahari Mngwali, Mbunge wa Mafia- viti maalum kwa tiketi ya Chama cha Wananchi- CUF amesema Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepoteza sifa yake, anaandika Pendo Omary.

Amesema kupoteza sifa kwa Bunge kunatokana na Bunge lenyewe kukosa hadhi ya kuwa mhimili unaojitegemea badala yake kufanya kazi kama wakala wa serikali.

Riziki ambaye ni kiongozi wa wabunge wa CUF bungeni amesema “niliingia bungeni kwa hamu kweli. Nikidhani ni chombo kikubwa kinachowakilisha wananchi na kinachofanya maamuzi kwa kujitegemea lakini nimekatishwa tamaa.”

“Nilitarajia sisi ni wawakilishi wa wananchi na msimamizi wa serikali. Yale mamlaka ya kikatiba ya Bunge siyaoni katika bunge hili. Mfano sisi wabunge wa upinzania tunavyoihoji serikali au kuishauri mara nyingi kiti cha spika au wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanatumika kuitetea. Sio wajibu wao,” anaeleza Riziki.

Mbali na Bunge kutumiaka kama wakala wa serikali, Riziki amesema mbunge mmoja mmoja hapewi hadhi inayotakiwa kama mwakilishi wa mamilioni ya wananchi badala yake hata hukumu dhidi yake zinatolewa kama mtu binafsi.

Soma mahojiano zaidi katika gazeti la MwanaHALISI la Jumatatu wiki ijayo.

error: Content is protected !!