Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wizara ya ardhi yazindua “ardhi app” kuwahudumia wananchi
Habari za Siasa

Wizara ya ardhi yazindua “ardhi app” kuwahudumia wananchi

Spread the love

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imezindua mfumo rasmi wa kuwahudumia wananchi popote walipo kupitia simu ya kiganjani “Ardhi App” wa kuwasilisha malalamiko ama migogoro ya ardhi katika wizara hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akizindua mfumo huo leo tarehe 22 Desemba 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wake na Wahariri wa Vyombo vya Habari kupitia Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Waziri  wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa  mesema, mfumo huo ni rafika na utawarahisishia wananchi kupata huduma wakiwa katika maeneo yao popote walipo.

“Mfumo huu wa “Ardhi App” utakuwa msaada mkubwa sana kwa wananchi wetu, utapunguza gharama na muda wa wananchi kupata huduma katika maeneo mbalimbali nchini, badala yake mwananchi atapata huduma za ardhi kiganjani mwake” amesema Waziri Silaa.

Kwa mujibu wa Waziri Silaa, mfumo huo pia utawasaidia wananchi kutoa mrejesho wa ubora wa huduma walizopatiwa pamoja na kuwasilisha tena malalamiko husika pale ambapo hawajaridhika  na majibu ama jinsi walivyohudumiwa.

Aidha, ameuelezea mfumo huo kuwa ni rafiki na utasaidia wananchi kuambatisha nyaraka na vielelezo vya malalamiko yao na kuondoa upotevu wa nyaraka pamoja na kupunguza urasimu katika kuwahudumia wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Timotheo Mzava amesema uzinduzi wa mfumo huo ni moja ya maboresho makubwa yanayofanywa na Wizara ya Ardhi  katika kuwahudumia wananchi kwenye sekta ya ardhi.

Uzinduzi huo umeshuhudiwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Geophrey Pinda, Katibu Mkuu Mhandisi Anthony Sanga, Naibu Katibu Mkuu, Lucy Kabyemera, wajumbe wa menejimenti wa wizara hiyo pamoja na wahariri wa vyombo vya Habari nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!