December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Mkuu Majaliwa mgeni rasmi Siku ya Vijana Duniani

Dk. Majaliwa Marwa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari

Spread the love

KASIM Majaliwa, Waziri MKuu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi leo katika Maadhimisho ya Siku ya Vijana duniani, ambapo kitaifa yanafanyika jijini Dodoma. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Siku ya Vijana duniani huanza kuadhimishwa tarehe 13 Agosti na kilele chake kuwa tarehe 16 Agosti kila mwaka. Maadhimisho hayo  yanatarajiwa kuhudhiwa na vijana 500 kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Akisoma taarifa ya pamoja kwa waandishi wa habari Dk. Maliwa Marwa, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN) amesema, vijana pamoja na serikali, Mashirika ya UN, Mashirika ya Kiraia ya Kimataifa na ya nchini, Taasisi za Elimu na Vyama vya Hiari kwa pamoja watahudhuria.

Amesema, maadhimisho yam waka huu ni ya 20 kufanyika tangu kuanzishwa kwake ambapo dhamira yake kwa Tanzania ni kuhakikisha mwaka 2030, Tanzania inakuwa ya viwanda na kuboresha elimu ya vijana kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

“Dhamila hii ,imechanganya msisitizo wa kimataifa katika kubadilisha elimu na kuifanya iwe jumuishi zaidi, inavyopatikana na umuhimu kwa dunia ya leo na ajenda ya taifa ya kuwa nchi yenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 na msisitizo maalum kwenye maendeleo ya viwanda.

“Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, inaangalia pia jinsi serikali, vijana na mashirika yanayoongozwa na vijana na yanayowalenga vijana pamoja na wadau wengine wanavyobadilisha elimu na jinsi juhudi hizo zinzvyochangia mafanikio ya ajenda ya mwaka 2030 ya Maendeleo Endelevu,” ameeleza Dk.Marwa.

error: Content is protected !!