December 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Video ya Mbowe: Ni kusuka au kunyoa

Spread the love

SWALI ni je, video iliyopokewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ikidaiwa kuonesha matukio yanayomuhusu Freeman Mbowe na wenzake kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Kinondoni 201 8 itaoneshwa? Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Katika kesi hiyo namba 112 ya uchochezi, Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)-Taifa, yeye na wenzake wanane wanatuhumiwa kufanya uchochezi wa uwasi na kufanya maandamano.

Katika maandamano hayo yaliyofanyika Februari 2018, yanadaiwa kusababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), Akwelina Akwilin.

Kuoneshwa ama kutooneshwa kwa video hiyo, kunategemea uamuzi wa Hakimu Thomas Simba, Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo kutokana na mvutano uliotokea kati ya pande mbili-Jamhuri na utetezi.

Watuhumiwa wengine kwenye kesi hiyo ni Dk. Vicent Mashinji, Katibu Mkuu-Taifa; John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu – Bara na Salumu Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu -Zanzibar.

Pia wamo Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini; Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Ester Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini; John Heche, Mbunge wa Tarime Vijijini na Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini.

Video hiyo ilitolewa tarehe 26 Julai 2019 mahakamani hapo ikiwa ni kielelezo namba tano Mid-Div (tepu za kurekodia) na kile namba nne (kamera), iliyodaiwa mahakamani hapo kurekodiwa na shahidi namba sita (Kolpo Charles) ambaye ni mpiga picha wa wa Jeshi la Polisi).

Upande wa Jamhuri katika kesi hiyo unawakilishwa na Faraja Nchimbi, Wakili wa Serikali Mkuu; Paul Kadushi, Wakili wa Serikali Mkuu na Wankyo Simoni, Wakili wa Serikali Mwandamizi.

Upande wa utetezi unaongozwa na Profesa Abdallah Safari akisaidiwa na Peter Kibatala, John Mallya na Hekima Mwasipu.

Tarehe 26 Julai mwaka 2019, mbele ya Hakimu Simba, upande wa mashtaka uliomba kamera kuwa kielelezo namba nne na namba tano (tepu).

Mahojiano ya mwisho kati ya Wakili wa Jamhuri na shahidi wao yalikuwa hivi;-

Wakili Kadushi: Kielelezo namba nne ni kielelezo gani?

Shahidi: Video kamera.

Wakili Kadushi: Hivi vielelezo namba 5 ni kitu gani?

Shahidi: Min-Div.

Wakili Kadushi: Wakati unaopiga picha za video hizi Min-Div zinakuwa wapi.

Shahidi: Ndani ya kamera.

Wakili Kadushi: Kwa muktadha huo unapopiga picha za video kumbukumbu zinahifadhiwa wapi kati ya kielelezo namba nne na namba tano?

Shahidi: Namba tano Min-Div.

Wakili Kadushi: Sasa shahidi wakati unatoa ushahidi uliiambia mahakama kuna namna mbili ya kutazama picha kwenye hii kamera na ukasema kwa namna ya kwanza unacheza video kupitia kamera yenyewe kupitia kitu gani?

Shahidi: LCD.

Wakili Kadushi: Lakini umesema kuwa kifaa kingine kinaweza kuonesha picha sauti ikiwa kubwa na sauti ikiwa kubwa ni sahihi?

Shahidi: Sahihi.

Wakili Kadushi: Uliambia mahakama hii kitendo cha kuitazama video kutoka kwenye kamera hii kwa chanzo cha pembeni hakiathiri kwa namna yoyote ya uhalisia wa video hiyo?

Shahidi: Sahihi.

Wakili Kadushi: Kwa namna gani mahakama inaweza kuangali video hizo?

Shahidi: Kutoka kwenye kamera kwenda kwenye screen au Projector kupita nyaya ya HDMI.

Wakili Kadushi: Kwa mujibu wa maelezo ya shahidi namna ambayo ametoa ushahidi wake mahakama inaweza kuangalia ushahidi kupitia screen kupitia nyaya ya HDMI tunaiomba Mahakama hii njia wezeshi ili kumbukumbu za ushahidi zilizokuwepo kwenye kielelezo namba tano zionekane kwa maana ya kisheria.

Kadushi ameendelea kuisitiza mahakama kupata mazingira wezeshi kwa ajili ya mahakama kuiona video.

Kibatala alipinga kuoneshwa kwa video hiyo kwa kuwa utaratibu wa kuionesha mahakama ushahidi huo ni wajibu wa upande huo uandae mazingira aidha kwa kuimbia mahakama ihamie kwenye mazingira wezeshi au wenyewe kuja na Projecta kwa ajili ya kuonesha video.

Alieza kuwa hata hizo nyanya za kuonyesha video hizo hazijatajwa kwenye ushahidi.

Alisisitiza hata chaji ya kamera hiyo lazima isitoke nje lazima iwe imetaja kwenye ushahidi.” Kwa hiyo sisi hata wangeomba waya ya kuchajia mahakamani tungepinga … kwa sababu hayo hayajafanyika tunaomba kielelezo namba nne na namba vichukuliwe kama vilivyo.

“Tunapinga chochote kufanyika kwa vielelezo hivyo vinginevyo shahidi aendelee kuelezea maelezo ya vielelezo hivyo,” alieleza Kibatala.

Wakili Kadushi alileza kuwa amesikia hoja za upande wa utetezi na kwamba hoja zote mbili zilizotolewa na Kibatala sio hoja za kisheria zinazokidhi matakwa ya kisheria.

“Ili pingamizi liwe pingamizi kisheria ni lazima lianishe kifungo cha sheria au sheria fulani itakayoielekeza mahakama … yote aliyoyaongea ni maoni binafsi,” alieleza Kadushi.

Alidai kuwa hatua aliyoieleza Kibataka washaipita na kwamba vielelezo vishapokelewa pia hoja ya kuwa watapinga hata wakileta waya wa chaji sio kile kinachotolewa mahakamani ni lazima kiwe ushahidi na alichosema kwamba tungeomba ukumbi wa mikutani huo sio utaratibu wa kisheria hoja hiyo inakinzana na hoja yake mwenyewe ya kwamba mazingira tuyaandae wenyewe wakati huo huo anasema tungeomba ukumbi wa mikutano ambao upo chini ya idara ya Mahakama.

“Ni rai yetu kwamba hoja ya kwamba tungeomba jengo la utawala sio jukumu letu na miundombinu yote inapaswa kuwa chini ya mahakama wenyewe ni jukumu la mahakama kuandaa mazingira ya kusikiliza ushahidi kwa muktadha huo tunarejea ombi letu Mahakama iwezeshe vielelezo visomwe au vioneshe,” alidai Kadushi.

Alieleza kwa vile nyanya au chaji sio kitu muhimu kwenye kupokelewa ushahidi huo.

Kibatala alidai kupeleka maombi mahakamani ni maombi ya kimahakama na sio maombi ya kiutawala na kwamba maombi ya kiutawala yanautaratibu wake.

Alidai kuwa shahidi aliieleza mahakama kuwa ili hiyi video ionekane kwenye screen lazima awe na nyaya ameiita (fire), ambayo haikutajwa mahakamani kama ilivyoelezwa kielelezo cha tano.

Profesa Safari alieleza mahakamani hapo kwa mfano ingekuwa kesi ya madai ilhali mahakama imetoa mazingira ya ushahidi tungesema mahakama imependelea.

Baada ya mabishano makali ya kisheria ya pande zote mbili Hakimu Simba ameihalisha kesi hiyo na kusema kwamba kesi hiyo inatakiwa iendeshwe haraka kwani sasa ishafika mwaka na nusu kwani imeenza Mwezi Machi Mwaka 2018 hivyo anataka kuendelea kusikiliza mfulilizo.

Uamuzi huo ulitarajiwa kutolewa tarehe 5 Agosti 2019 ambapo pia kesi hiyo ingesikilizwa mfululizo hadi tarehe 6 na 7 Agosti 2019, lakini Hakimu Simba aliahirisha mpaka tarehe 15 Agosti 2019 kwa sababu ya kufiwa kwa kaka wa mshtakiwa wa nane (Heche).

error: Content is protected !!