November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Makamba azungumzia uhaba dizeli, petroli

January Makamba, Waziri wa Nishati na Madini

Spread the love

 

WAZIRI wa Nishati nchini Tanzania, January Makamba amesema, mafuta ya dizeli yaliyopo kwenye matenki yanatosheleza kwa siku 24 huku petrol ikiwa ya siku 34. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Makamba ameelezea uwepo wa nishati hiyo leo Ijumaa, tarehe 12 Novemba 2021, kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Twitter. Ni baada ya uwepo wa taarifa kwamba kuna upungufu wa mafuta nchini humo.

“Hakuna uhaba wa mafuta nchini. Hakuna sababu ya kuwa na taharuki. Utaratibu wa kuingiza mafuta unahakikisha kwamba mahitaji yapo wakati wote. Serikali inaendelea kuchukua hatua kuongeza uhakika wa upatikanaji na unafuu wa bei,” amesema.

Makamba amesema, Dizeli iliyopo kwenye matenki nchini hadi leo asubuhi ni lita milioni 90.7. Meli inayoitwa SLOANE SQUARE muda huu inashusha lita milioni 60.9 hivyo kupelekea mafuta ya dizeli kuongezeka na kuwa lita 151,694,926 yanayotosheleza kwa siku 24.

Mbunge huyo wa Bumbuli mkoani Tanga amesema, petroli iliyopo kwenye matenki nchini hadi leo asubuhi ni lita 100,345,631. Meli iitwayo JAMES COOK inashusha lita 22,493,188; meli iitwayo JAG PUNIT iko njiani na lita 30,579,019 hivyo kupeleka mafuta ya petroli kuongezeka na kuwa lita 153,417,838 yanayotosheleza kwa siku 34

error: Content is protected !!