December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Miezi tisa: Watoto 6,168 wafanyiwa ukatili Tanzania

Baadhi ya watoto waliofanyiwa ukatili

Spread the love

 

WIZARA ya Mambo ya Ndani nchini Tanzania, imesema kuanzia Januari hadi Septemba 2021, takwimu ya vitendo vya ukatili kwa watoto vilivyoripotiwa vituo vya Polisi inaonesha watoto 6,168 wamefanyiwa ukatili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Ijumaa, tarehe 12 Novemba 2021 na naibu waziri wa wizara hiyo, Khamis Hamza Chilo wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum, Esther Matiko.

Matiko ameuliza, ukatili kwa watoto umekithiri nchini kama vile ubakaji, ulawiti, kuchomwa moto na mimba za utotoni.

“Je ni watoto wangapi wamefanyiwa ukatili huo kwa jinsia zao wa kike na wa kiume na je, kuna takwimu halisi ya hatua zilizo chukuliwa na Serikali dhidi ya matukio hayo nchini,” ameuliza mbunge huyo.

Ajibu swali hilo, Chilo amesema, kati ya watoti hao waliofanyiwa ukatili, wanawake 5,287 na wanaume 881.

Amesema, waliobakwa ni 3,524, waliolawitiwa ni 637 kati yao wanaume 567 na wanawake 70, waliochomwa moto ni 130 kati yao wanaume 33 na wanawake 97, waliopata mimba ni 1,877.

Naibu waziri huyo amesmea, kesi na watuhumiwa waliokamatwa na kufikishwa mahakamani ni 3,800.

“Kesi zilizo chini ya upelelezi ni 2,368 na kesi zilizohukumiwa ni 88 na nyingine ziko kwenye hatua mbalimbali mahakamani,” amesema Chilo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Khamis Hamza Chilo

Akiuliza maswali ya nyongeza, Matiko amesema, “kwa takwimu tu za serikali, inaonesha ukatili kwa watoto ni mkubwa. Hizi takiwmu ni Januari hadi Septemba, ingekuwa ya miaka mitano ingekuwa.”

Ni utaratibu gani umewekwa ili kuwa na takwimu kutoka vyanzo mbalimbali?
Akijibu swali hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama amesema, kumekuwa na mkakati wa kupambana na ukatili na unyanyasaji kwa wanawake na watoto.

Mhagama amesema, mkakati wa kwanza unakwenda kumalizika “na hivi karibuni tulikuwa katika kikao kufanya tathimini ya hali ilivyo. Lakini nimhakikishie mbunge, mkakati wa pili utakuja na suluhisho ikiwemo bajeti na mengine yatazingatiwa.”

error: Content is protected !!