May 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Waziri Jafo: Hakuna binadamu aliyekamilika, lazima tuvumiliane

Seleman Jafo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (TAMISEMI)

Spread the love

KUELEKEA Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano 28 Oktoba 2020, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo amewataka viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani katika nyumba za ibada. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea)

Waziri Jafo amesema hayo leo Jumapili tarehe 30 Agosti jijini Dodoma wakati akifungua semina elekezi kwa viongozi wa dini kuhusu amani kuelekea uchaguzi mkuu.

Semina hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Markaz Islaam ya Chang’ombe jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Dodoma.

Waziri Jafo amesema, amani ni muhimu kipindi hiki nchi ikielekea katika uchaguzi mkuu.

“Twendeni tukahubiri amani, hakuna binadamu ambaye aliyekamilika ila lazima tuvumiliane, tupime nia za watu, tuna kila sababu ya kuendelea kupendana.”

“Viongozi wa kisiasa nao wanawajibu wa kuendelea kuhubiri amani. Mataifa yote yanayotuzunguka yote yamepata misukosuko, ukienda hapo Kongwa unaona Kambi tulikuwa tunawalea, sisi Tanzania tunawajibu wa kuendelea kulinda amani,” amesema Jafo

“Bahati mbaya kila mtu ana urefu wa kamba yake, amani ikiharibika kesho hayupo, mwenzangu na mimi umejitahidi sana umeenda Chemba, mwingine kakimbilia Kondoa, mwenzako ana passport mbili mambo yakiharibika tu huyoo,” amesema Jafo.

Waziri Jafo amewaomba, Maimamu wa Misikiti wawe wanaweka kipengele cha kuhubiri amani kwa waumini wao wakati wa ibada ya swala ya Ijumaa wakati huu Tanzania ikielekea katika uchaguzi mkuu.

“Agenda ya amani ni msingi wa kila kitu, tuna siku kadhaa za kwenda katika uchaguzi mkuu, fursa hii inatakiwa pia kuwepo katika hotuba za maimamu tuwe tunaweka kipendele cha amani.”

“Amani inapopotea watu wenye vyeo vyao wanakuwa madhalili, matajiri wanakuwa masikini mfano Libya ya zamani na sasa lakini tuangalie Libya ilivyo sasa, mabwana wamegeuka kuwa watwana,” amesema

“Bila amani mke wako atadhalilishwa mbele yako, amani ndio jambo kubwa sana katika maisha ya binadamu angalia ndugu zetu wa Yemeni, Syria, Jamhuri ya Afrika ya Kati kila mtu analala kwenye nyumba yake hajui kama kesho ataaamka,” amesema.

Waziri Jafo ambaye anagombea Ubunge Kisarawe kupitia CCM amesema, amani ikipotea uchumi wa nchi utayumba hivyo kila mmoja anawajibu wa kuilinda.

“Bahati mbaya maadui wanaingiza mambo yao wakati wa Uchaguzi kipindi hichi viongozi wa dini mnapaswa kusimamia amani,mnapaswa kuzifanya roho za binadamu ziwe na utu.

“Amani ikiondoka hakuna kufanya kazi, amani inaenda sambamba na uchumi kama kuna watu wana nia mbaya kuja kuharibu uchumi,” amesema

Awali, Sheikhe wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Rajabu alisema kazi za kijamii zinahitaji ushirikiano mkubwa na dini zote zinatakiwa kushirikiana.

“Jukumu la kulinda amani ni letu sote, Mwenyezimungu hajawakata kushirikiana, yapo mambo sisi kama Waislamu tunaweza kushirikiana nayo na miongoni mwao ni ujamii ambayo hatuwezi kushirikiana ni masuala ya kiitikadi na kiibada.Unaweza kushirikiana katika ugonjwa, kukopeshana, kuishi pamoja,” alisema

Sheikhe Rajabu aliwataka Masheikhe wa Misikiti kuhubiri amani huku akitaka kutoruhusu nyumba za ibada kutumiwa na wanasiasa kufanya kampeni katika misikiti.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Markaz Islaam Chang’ombe Dar es Salaam, Dk.Kamal Abdul Mut’wi alisema lengo la semina hiyo ni kueneza amani pamoja na kuonesha mtazamo wa amani kwa Waislamu.

error: Content is protected !!