Wednesday , 21 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mke wa Lissu alivyomwombea kura mmewe
Habari za Siasa

Mke wa Lissu alivyomwombea kura mmewe

Spread the love

ALICIA Magabe, mke wa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amewaomba Watanzania kutafakari miaka mitano iliyopita na kuamua katika Uchaguzi Mkuu ujao utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea)

Alicia alitoa wito huo jana Jumamosi tarehe 29 Agosti 2020 katika mkutano wa kampeni za urais wa Tanzania uliofanyika Uwanja wa Tanganyika Packers uliopo Jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mamia ya wananchi na wanachama wa Chadema waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo, Alicia alianza kwa kusema “sijui nianzie wapi” huku sauti sikisikika zikisema “anzia hapo hapo”

“Mimi naomba nianze kwa kuwashukuru sana kwa sababu siku ile ya tarehe 7 Septemba (2017), ubavu wangu ulimiminiwa risasi 16 na tangu siku ile maisha yetu yalibadilika.”

Huku uwanja ukiwa kimya kumsikiliza, Alicia akasema “ninyi mnafahamu” kilichomtokea.

Siku hiyo aliyoizungumza, Lissu alishambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 kati ya hizo 16 zilimpata mwilini na watu wasiojulikana akiwa anataka kushuka kwenye gari nyumbani kwake Area D jijini Dodoma akitoka kuhudhuria kikao cha Bunge.

Mara baada ya kushambuliwa, alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na usiku wa siku hiyohiyo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya kwa matibabu zaidi.

Tarehe 6 Januari 2018, Lissu na mkewe, Alicia walihamia nchini Ubelgiji kuendelea na matibabu na baada ya kupona akarejea nchini 27 Julai 2020.

Akiendelea kuwahutubia wananchi uwanja hapo, Alichia alisema “mimi, mme wangu Tundu na watoto wetu, Kawe ni nyumbani, tunaishi Tegeta tangu mwaka 1997 tulipofunga ndoa, hatujawahi kuhama japo tunamji mwingine Magambwe Singida.”

“Kawe ni kwetu, Dar es Salaam ni kwetu, Tanzania ni kwetu. Niwashukuru sana kwa namna ya kipekee mlikuwa nasi tangu siku ile ya tukio baya mpaka sasa. Hatuna jinsi ya kuwalipa Kawe,” alisema

Alicia ambaye kitaalum ni mwanasheria alisema “ila na mimi naomba tukienda kwenye kupiga kura, tuwe tunayakataa maovu yote yaliyotokea kuanzia Oktoba ile ya uchaguzi wa mara ya mwisho (uliofanyika 25 Oktoba 2015). Uamuazi ni wetu.”

jana ilikuwa siku ya pili ya uzinduzi wa kampeni za uchaguzi za chama hicho ambapo Ijumaa zilianzia Uwanja wa Zakhiem, Mbagala Dar es Salaam.

Alicia akizungumza kwenye viwanja wa Mbagala alisema “sina mengi ya kuzungumza, ila nawashukuru wote kwa hali na mali kwa support yenu kipindi ambacho mme wangu kipenzi alipokuwa anaumwa ambaye sasa hivi anaweza kusimama na kugombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungamno wa Tanzania.”

Leo Jumapili, Lissu atahitimisha uzinduzi kwa siku ya tatu kwenye mkutano utakaofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Liwili- Tabata.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Mwinyi ateua waziri wa uchumi na uwekezaji Zanzibar

Spread the loveRAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi,...

Habari za SiasaTangulizi

Mvua yakatisha mkutano wa Chadema Mbeya

Spread the loveMKUTANO wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),...

Habari za Siasa

Sugu atumia maandamano ya Chadema kumfikishia ujumbe Spika Tulia

Spread the loveALIYEKUWA Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi “Sugu”, ametumia maandamano...

Habari za SiasaTangulizi

Sakata la DP World na bandari lafufuka upya

Spread the loveSAKATA la mkataba wa kiserikali kati ya Tanzania na Imarati...

error: Content is protected !!