Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waziri hajui gharama za kukimbiza Mwenge
Habari za Siasa

Waziri hajui gharama za kukimbiza Mwenge

Askari wakiulinda Mwege wa Uhuru
Spread the love

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ameshindwa kujua bajeti ya ukimbizaji wa mbio za Mwenge kwa nchi nzima kwa kipindi cha mwaka mmoja, anaandika Dany Tibason.

Waziri alionesha udhaifu huo kutokana na kushindwa kujibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nkasi, Ally Keissy (CCM) aliyetaka kujua ni kiasi gani cha fedha utumika katika kukimbiza mbio za Mwenge nchi nzima kwa mwaka.

Naye mbunge wa Magogoni, Dk. Suleimani Ally Yussuf (CUF) akiuliza swali la nyongeza bungeni alitaka kujua ni kwanini serikali inawalazimisha Wazanzibari kukimbiza mwenge wakati kwa imani yao wanaamini kuwa mbio za Mwenge ni ibada ya kuabudu moto.

Mbunge wa Konde, Khatibu Said Haji (CUF) akiuliza swali la nyongeza naye alitaka kujua iwapo Mwenge kusudio lake ni umoja, upendo na mshikamano ni kwanini umegeuka kueneza chuki kwa kuwaadabisha au kuwaweka mahabusu baadhi ya wenyeviti wa mitaa kutokana na kushindwa kuchangisha fedha za mbio za mwenge.

“Kwa kuwa Mwenge siyo jambo la Muungano, Je ni kwanini Mwenge ukimbizwe Zanzibari wakati hata Zanzibar nayo ina historia ya kupata uhuru wa mapinduzi,” alihoji Haji.

Awali katika swali la msingi la mbunge huyo wa konde alitaka kujua kama kuna faida kwa watanzania kuendelea kukimbiza Mwenge wa Uhuru kila mwaka na kama faida zipo ni faida gani?

Pia alitaka kujua kama hakuna faida ya kuwepo kwa mbio za Mwenge wa Uhuru, na ni lini utasitishwa.

Akiaza kujibu maswali ya nyongeza ya wabunge akianza na swali la Keissy amesema kuwa bajeti ya mbio za Mwenge uandaliwa na halmashauri husika kwa lengo la kufanikisha mbio hizo.

Akiju swali la nyongeza la mbunge wa Magogoni, waziri amesema pamoja na kuwepo kwa imani ya kila mmoja lakini mwenge una historia ndefu ya uhuru hivyo mwenge huo utaendelea akukimbizwa ndani ya Tanzania Bara na visiwani Zanzibar.

Pia amesema katika kuendelea kukimbiza mwenge serikali itajitahidi kuondoa dosari mbalimbali ambazo zinaonekana kujitokeza ili pasiwepo na matatizo yoyote.

Akijibu swali la msingi Mhagama amesema faida za Mwenge wa Uhuru kitaifa na kimataifa ni pamoja na kuendelea kuhamasisha ari ya wananchi kujitegemea na kuwekeza katika maeneo mbalimbali katika taifa.

Aidha amesema Mwenge wa Uhuru ni chombo pekee cha kujenga umoja na mshikamano na kudumisha amani pale unapopita bila kujihusisha na itikadi za kisiasa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!