Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali: Bila kulipwa mtumishi asihame
Habari Mchanganyiko

Serikali: Bila kulipwa mtumishi asihame

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene
Spread the love

SERIKALI imepiga marufuku tabia ya baadhi ya wakurugenzi ambao wanawahamisha watumishi bila kuwa na bajeti ya kuwalipa fedha zao, anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, George Simbachawene alipokuwa akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalum, Kemilembe Lwota (CCM).

Katika swali la nyongeza mbunge huyo alitaka serikali ieleze ni lini italipa madeni yote ya uhamisho kwa watumishi waliohamishwa bila kulipwa fedha zao.

Awali katika swali la msingi la mbunge huyo alitaka kujua ni lini serikali itawalipa stahiki zao watumishi wanaohamishwa bila kulipwa fedha zao za uhamisho.

“Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa ni miongoni mwa halmashauri mpya zilizoanzishwa mwaka 2015 na watumishi 98 walihamishwa kutoka katika halmashauri za Sengerema, Misungwi, Ilemela, Jiji la Mwanza, Kwimba na Magu lakini watumishi hawa hadi sasa hawajalipwa fedha za uhamisho.

“Je ni lini serikali itawalipa stahiki zao watumishi hao waliohamishwa bila kupatiwa stahiki zao kama inavyotakiwa” alihoji Lwota.

Akijibu swali la nyongeza Simbachawene amesema ni marufuku kwa wakurugenzi wote nchini kuwahamisha watumishi hususani walimu bila kuwa na bajeti ya kuwalipa fedha zao za uhamisho.

Mbali na hilo amesema wakurugenzi ambao watakuwa wameshindwa kuwalipa fedha zao za uhamisho watumishi waliohamishwa kati ya Januari hadi Machi hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wakurugenzi hao.

“Nimeisha toa maagizo kuwa ifikapo mwezi Aprili 30 mwaka huu wale wote ambao walihamishwa kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Aprili wawe wamelipwa fedha zao,” alisema Simbachawene.

Mbali na hilo amesema utaratibu na uhakiki wa madeni kwa watumishi waliohamishwa unaendelea kufanyika ili kuhakikisha wanalipa madeni hayo kwa watumishi waliohamishwa bila kulipwa fedha zao za uhamisho.

Akijibu swali la msingi Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Seleman Jafo amesema Halmashauri ya Buchosa ni miongoni mwa halmashauri zilizoamishwa Julai, 2015 baada ya kugawanywa kwa halmashauri ya Sengerema.

Watumishi 98 waliohamishwa Buchosa kutoka halmashauri za Sengerema, Ilemela, Jiji la Mwanza, Kwimba na Magu wanadai jumla ya Sh. 354,075,500 na kati ya hizo tayari madai ya Sh. 44,531,000 yamelipwa kwa watumishi 16.

“Hadi Desemba mwaka jana halmashauri imebakiwa na madeni ya uhamisho wa watumishi 88 yenye jumla ya Sh. 292,531,000 madeni hayo yamewasilishwa Wizara ya Fedha na Mipango kwa ajili ya uhakiki ili yaweze kulipwa,” alieleza Jafo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!