Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wazamiaji Afrika Kusini wadakwa, wafikishwa Kisutu
Habari Mchanganyiko

Wazamiaji Afrika Kusini wadakwa, wafikishwa Kisutu

Spread the love

WATANZANIA 30 waliorudishwa nchi kutoka Afrika Kusini, walikokuwa wakiishi kinyemelea, wamefikishwa katika Mahakama ya Kisutu, kujibu tuhuma za kusafiri kinyume cha sheria. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Watuhumiwa 16 kati yao, leo tarehe 23 Januari 2020, wamesomewa mashtaka na wakili wa serikali, kutoka Idara ya Uhamiaj, Godfrey Ngwijo mbele ya hakimu mkazi Mwandamizi Augustine Mmbando.

Wanadaiwa tarehe 21 Januari 2020, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), walikutwa nje ya nchi bila kufuata Afrika Kusini kinyume na taratibu za uhamiaji.

Washitakiwa wote walikubali mashitaka, ambapo upande wa mashitaka uliwasomea maelezo ya awali,

Upande wa mashtaka umedai, tarehe zisizofahamika watuhumiwa walitoka Tanzania na kuingia Afrika Kusini bila kufuata taratibu.

Ngwijo alidai katika tarehe hiyo, washitakiwa walikamatwa nchini humo na kuletwa Tanzania na kwamba, walifikishwa JNIA kisha kupelekwa Ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam kuchukuliwa maelezo.

Washtakiwa hao wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miezi sita gerezani, ama kulipa faini ya Sh. 300,000 kila mmoja.

Baadhi yao wamefanikiwa kulipa faini na wamechukuliwa na wazazi wao.

Washitakiwa hao ni Omary Kaulu, Dominic Fabric, Sefu Mohammed, Hamad Hashiri, Asbawi Omar, Abdala Hamad, Razan Ally, Moosa Salimu, Mawki Ally, Daniel Joshua, Amari Abduli, Abdullah Ramadhan, Mohammed Tuwa, Aziz Mohammed, Rajabu Shabani na Adam Seifu.

Hata hivyo, washitakiwa hao kwa nyakati tofauti waliomba mahakama iwapunguzie adhabu, kwasababu wamekaa sana gerezani walipokuwa Afrika Kusini.

Washtakiwa wengine ni Adam Luzz, Suleiman Saidi, Kapaya Fredric, Semboko Abubakari, Mambosasa Francis, Juma Muhina, Chale Othoman, Salehe Iddy, Mohammed Kassim, Hassan Ally, Boban Abed, Abdul Kessy, John Joseph na Mawazo Frank ambao wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Salum Ally.

Washtakiwa hao wamehukumiwa kulipa faini ya sh.50,000 ama kwenda jela miezi 18.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!