April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Zungu aukwaa uwaziri, Simbachawene amrithi Lugola

Spread the love

RAIS John Magufuli amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri, kwa kumteua Mussa Zungu, Mbunge wa Ilala kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira, akichukua nafasi ya George Simbachawene. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mabadiliko hayo yametangazwa leo tarehe 23 Januari 2020, na Katibu Mkuu  Kiongozi Ikulu, Balozi John Kijazi.

Kwa mujibu wa Balozi Kijazi, Simbachawene aliyemhamishia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, amechukua nafasi ya Kangi Lugola, ambaye uteuzi wake umetenguliwa leo na Rais Magufuli.

Wakati huo huo, Rais Magufuli ameteua mabalozi watatu, akiwemo Jenerali Jacob Kingu, aliyejiuzulu Ukatibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kuwa Balozi.

Balozi Kijazi amesema  vituo vya kazi vya mabalozi hao, vitatangazwa baadae.

Pia, Balozi Kijazi amesema Rais Magufuli amewaongezea muda wa miaka 2, mabalozi saba, akiwemo Asha Rose Migiro, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, George Madafa Balozi wa Tanzania nchini Italia na Emmanuel Nchimbi (Brazil).

error: Content is protected !!