Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wawili mbaroni tuhuma za kuiba vyuma daraja la Tanzanite
Habari Mchanganyiko

Wawili mbaroni tuhuma za kuiba vyuma daraja la Tanzanite

Spread the love

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kujaribu, kukata baadhi ya vyuma vya ngazi ya nguzo kwenye daraja la Tanzanite lililopo maeneo ya Salender jijini hapa. Anaripoti Rhoda Kanuti …(endelea).

Watuhumiwa hao ambao majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi, walikamatwa tarehe 2 Aprili, 2022 saa 10 alfajiri wakiwa wanajaribu kufungua vyuma vilivyopo kwenye nguzo inayojulikana kama P9 ambayo ipo kwenye daraja hilo.

Akizungumza na wanahabari leo Jumatatu tarehe 4 Aprili, 2022 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema watuhumiwa hao wanahojiwa kwa kina na watafikishwa kwenye vyombo vya kisheria kwa hatua zaidi pale uchunguzi utakapokamilika.

Aidha, amesema Jeshi hilo limewakamata watu wengine kumi waliokutwa chini ya daraja hilo, wakidai kuwa wanaokota vyuma chakavu kwa ajili ya biashara ya vyuma.

“Watuhumiwa hao pia wanahojiwa kwa kina ili kubaini malengo yao chini ya daraja hilo, yalikuwa ni nini na kuona kama wana uhusiano na wale waliokuwa wanajaibu kuiharibu baadhi ya miundombinu ya nguzo,” amesema Muliro.

Muliro ametoa onyo na kwamba halitamvumilia mtu au kikundi chochote kinachojihusisha kwa namna yoyote ile kujaribu kuharibu miundombinu ambayo imejengwa kwa manufaa ya umma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!