Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Prof. Mkenda awafunda vijana wanaotaka siasa
Habari Mchanganyiko

Prof. Mkenda awafunda vijana wanaotaka siasa

Spread the love

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolph Mkenda, amewataka vijana wasiingie katika siasa kwa ajili ya kutafuta maslahi yao binafsi, bali waingie kwa ajili ya kupigania maslahi ya Taifa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Prof. Mkenda ametoa wito huo leo Jumatatu, tarehe 4 Aprili 2021, akifungua kongamano la miaka 100 ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, lililofanyika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.

“Tusiingie kufanya siasa ni kinyang’anyiro cha kutafuta madaraka, mali na umaarufu, tuingie na kamoyo fulani ka-uanaharakati wa kujaribu kuleta maendeleo ya nchi yetu. Na Hiyo itaondoa ubabe ubabe kwenye siasa, ikaongeza ushawishi kwamba mwanasiasa kazi yake kubwa ni kushawishi,” amesema Prof. Mkenda.

Waziri huyo wa elimu, amesema Mwalimu Nyerere enzi anapigania uhuru wa Tanganyika na Afrika, hakuweka maslahi yake mbele, bali alijitosa katika harakati hizo kwa kuwa alitamani kuimarisha haki za binadamu.

“Mwalimu aliingia kwenye siasa kwa hamasa ya dhana aliyotaka kuipigania, sio umaarufu, tamaa ya mali wala madaraka. Sababu hata alivyochukua madaraka harakaharaka alikuwa anatamani aachie mwenyewe.

Alikuja kuachia madaraka mwenyewe hakualzimishwa,” amesema Prof. Mkenda.

Prof. Mkenda amesema kazi ya siasa ni ya kujitolea katika kuwaletea maendeleo wananchi na taifa kwa ujumla.

“Kazi ya siasa haibadiliki, lazima iwe na muelekeo wa kujitolea. Kwa namna fulani mwanasiasa utakuwa maarufu lakini isiwe sababu ya kuingia kwenye siasa.

“Siasa zetu tuhakikishe za kupigania maslahi ya wenzetu na ya nchi yetu katika kitu tunakiamini usawa wa binadamu, kila tunachojenga tutoe fursa bila ubaguzi,” amesema Prof. Adolph Mkenda.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Stephen Wasira, amesema Mwalimu Nyerere enzi za uhai wake alipigania usawa wa binadamu.

“Mwalimu alimama katika maisha yake yote aliamini katika usawa na maandiko yote aliyoandika alizungumza usawa wa binadamu na maendeleo. Akiamini katika umoja hata alipoanzisha TANU nia yake ni kuwaandaa Watanzania kujitawala,” amesema Wasira.

Wasira amesema, umoja wa Watanzania, ni zao la kazi ya Mwalimu Nyerere.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!