NASHON Bidyanguze, Mbunge wa Kigoma Kusini (CCM), amehoji lini watumishi waliohamishiwa halmashauri ya Uvinza kutoka Kigoma Vijijini watalipwa stahiki zao. Anaripoti Jemima Samwel, DMC … (endelea).
Bidyanguze amehoji hayo leo Ijumaa, tarehe 30 April 2021, bungeni jijini Dodoma, katika swali lake akisema, “je ni lini watumishi waliohamishiwa Halmashauri ya Uvinza kutoka Halmashauri ya Kigoma Vijijini watalipwa stahiki zao?”
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Tamisemi, David Silinde amesema, halmashauri ya Wilaya Uvinza ina watumishi 99, wanaostahili kulipwa stahiki za uhamisho kufuatia kuhamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kwenda Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza.
“Katika mwaka wa fedha 2013/14, kiasi cha Sh.319.89 milioni kinahitajika ili kullipa madeni hayo ya watumishi,” ameeleza Tamisemi.
“Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, ilipaswa kutenga fedha katika mapato yake ya ndani ili kulipa madeni hayo jambo ambalo halijafanywa takriban miaka minane.”
“Namuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, kutenga fedha katika mapato ya ndani ya Halmashauri na kulipa madeni hayo,” amesema Silinde
Leave a comment