May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Yanga yaipiga Prisons, yatinga robo fainali

Spread the love

 

USHINDI wa bao 1-0, limewatosha kuifanya Yanga, kutinga hatua ya robo fainali ya michuano Kombe la Shirikisho (FA Cup) dhidi ya Tanzania Prisons. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Mchezo huo umechezwa, leo Ijumaa, tarehe 30 Aprili 2021, Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga, mkoani Rukwa na kuifanya Prison kupoteza sifa ya kuendelea kwenye michuano hiyo.

Iliwachukua dakika 54, kwa Yanga kuandika goli la kwanza na la ushindi kupitia kwa Yacouba Sogne, aliyepokea pasi safi kutoka kwa Saido Ntibanzokiza.

Kwa matokeo hayo sasa, Yanga inafuzu kuelekea hatua inayofuata ya robo fainail.

Mara baada ya mchezo huo, Yanga itarejea Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba utakaochezwa tarehe 8 Mei 2021.

Kwenye mchezo wa leo, Yanga ilikosa huduma ya wachezaji wake sita kutokana na majeruhi huku wengine wakitumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Tuisila Kisinda, Dikson Job na Yassin Mustapha wao waliukosa mchezo kutokana na kupata majeruhi, huku Michael Sarpong, Mukoko Tonombe na Feisal Salum wao walikuwa wakitumikia adhabu ya kuwa na kadi tatu za njano.

error: Content is protected !!