February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

‘Watu wasiojulikana’ wavamia ofisi za gazeti waua watano

Mfano wa mtu aliyefanya mashambulizi katika Chumba cha habari cha gazeti la Capital Gazette la Marekani. Picha ndogo ofisi za gazeti hilo

Spread the love

WATU wasiojulikana wamevamia ofisi za gazeti la Capital Gazette na kufyatua risasi na kuua watu watano na kuwajeruhi wengine, katika jiji la Maryland, Marekani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mmoja wa wafanyakazi wa gazeti hilo amesema kuwa mtu aliyefyatua risasi katika chumba cha habari kupitia kwenye dirisha la vioo.

“Tukiwa kwenye madawati yetu katika chumba cha habari, tulistuka kusikia mtu akikoki bunduki na ghafla kuanza kusikia milio la risasi. Ni tukio la kustiha sana sana.” Aliandika mmoja ya waandishi walionusurika, Phil Davis katika ukurasa wake wa Twitter.

Polisi wameimarisha ulinzi katika eneo hilo na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

“Hili ni tukio baya sana lililotokea mchana huu,” alisema Mtendaji wa eneo hilo, Steve Schuh katika mkutano na waandishi wa habari. “Watu kadhaa wamefariki katika tukio hilo.”

Polisi wamesema kwa sasa hawawezi kutambua hasa ni aina gani ya silaha iliyotumika, lakini uchunguzi unaendelea wakisaidia na FBI na taasisi nyingine.

error: Content is protected !!