Monday , 26 February 2024
Home Kitengo Michezo Afrika wawaachia wenye mpira wao
MichezoTangulizi

Afrika wawaachia wenye mpira wao

Spread the love

KOMBE Dunia linaingia katika hatua ya mtoano bila kuwa na timu kutoka Bara la Afrika, baada timu zote tano kutolewa hatua ya makundi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika fainali za Kombe la Dunia 2018 Afrika iliwakilishwa na timu za Misri, Morocco, Tunisia, Nigeria na Senegal ambazo zote zimeaga katika hatua ya makundi.

Lakini ni machungu kwa bara hili kwani matumaini ya mwisho, Senegal, imeliaga Kombe baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 leo dhidi ya Colombia.

Juhudi za Senegal zinastahili kupongezwa kwani wawakilishi wengine wa Afrika walifunga virago mechi zao ya pili.

Mbali na Nigeria na Tunisia, Senegal ndiye mwakilishi mwingine wa Afrika kusajili ushindi mechi hatua ya makundi.

Kuanzia Jumamosi ijayo, timu 16 zitakuwa viwanja tofauti Urusi kusaka tiketi ya robo fainali.

Timu 16 zitakazowania tiketi ya robo fainali ni Uruguay, Urusi, Uhispania, Ureno, Ufaransa, Denmark, Croatia, Argentina, Sweden, Mexico, Brazil, Uswizi, Colombia, Japan, Ubelgiji na Uingereza.

Hata hivyo, miujiza si haba Kombe hili kwani mabingwa watetezi, Ujerumani tayari wametemwa baada ya kucharazwa 2-0 na Korea Kusini.

Kila taifa Afrika sasa lina majukumu ya kujiandaa kwa Qatar 2022 kwani wote wana nafasi sawa ya kufuzu!

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Wizara yaahidi kuboresha, kuimarisha michezo

Spread the loveIkiwa ni saa kadhaa baada ya kumalizika kwa mashindano ya...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari MchanganyikoMichezo

Nje jogging yanyakua medali 20 Kili Marathon

Spread the loveTimu ya riadha ya Wizara ya Mambo ya Nje na...

error: Content is protected !!