Monday , 26 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wateule wa Rais Magufuli wagonganishwa Dodoma
Habari za SiasaTangulizi

Wateule wa Rais Magufuli wagonganishwa Dodoma

Rais John Magufuli akiwa kazini
Spread the love

WAKULIMA wa Songambele “B ” wilaya ya Kongwa, Dodoma wamemtaka mkuu wa mkoa wa huo, Dk. Binilithi Mahenge kuingilia kati mgogoro kati ya wakulima na wafugaji unaidaiwa kukuzwa na mkuu wa wilaya ya Kongwa, Deogratias Ndejembi, anaandika Dany Tibason.

Wakulima hao wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari katika mashamba wanayolalamikia kuwa yamegeuka kuwa malisho ya ng’ombe wamesema kuwa kutokana na kuwepo kwa mgogoro wa muda mrefu kati ya wakulima na wafugaji huku mkuu wa wilaya akiwalinda zaidi wafugaji kunaweza kutokea machafuko.

Mwenyekiti wa wakulima Songambele “B” Sospiter Chiuyo, amesema kwa sasa hawana imani mkuu wa wilaya ya Kongwa juu ya mgogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Amesema ni muda mrefu sasa wamekuwa wakilalamika juu ya ukorofi unaofanywa na wafugaji lakini mkuu wa wilaya anapuuza.

Kutokana na hali hiyo mwenyekiti wa wakulima kwa niaba ya wakulima amesema anayeweza kutatua mgogoro huo ni mkuu wa mkoa Dodoma kwa maana tayari wameisha mpatia taarifa za mkuu wa wilaya kushindwa.

Aidha amesema kuna kila sababu ya kufanya uchunguzi ni kwanini mkuu wa wilaya ya Kongwa amekuwa akitaka kubadilisha natumizi ya ramani kwa kutaka kuwapendelea wafugaji kwa kuwapora wakulima maeneo yao ambayo wanayamiliki kisheria.

Naye Peter Enock ambaye ni katibu wa wakulima Songambele “B” amesema kutokana na kuwepo kwa mgogoro kati ya wafugaji na wakulima wameshindwa kuandaa mashamba licha ya kuwa msimu wa kilimo kukaribia.

Enock amewaeleza waandishi wa habari kuwa mkuu wa wilaya amekuwa kichocheo kikubwa cha kukuza mgogoro huo kwani ameshindwa kuwa na maamuzi licha ya kupatiwa malalamiko ya muda mrefu.

Katibu huyo alisema ramani ya Songambele “B” inaonesha wazi maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wakulima na wafugaji lakini anayelea kuwa wanashangazwa kuona mkuu wilaya kubadilisha matumizi ya ramani na maeneo ya kilimo kuwa ya wafugaji.

Naye Mhasibu wa wakulima Raid Mkotya amesema kuwa kama serikali ya mkoa haitaingilia kati mgogoro huo kuna uwezekano damu ikamwagika.

“Kwanza ifahamike wanaoleta mifugo katika mashamba ya wakulima wa Songambele siyo wenyeji bali wanatoka, Gairo, Ngomai na Silalahi wamekuja hapa zaidi ya shamba la mbaazi heka mia wamelisha ukiwaambia wanakuja juu na kusema wana kibali cha mkuu wa wilaya,” amesema mhasibu.

Naye Rosse Mangula ambaye ni mkulima wa Songambele “B” amesema kuwepo kwa mgogoro kati ya wakulima na wafugaji usiohisha unaweza kuhatarisha maisha Kati ya jamii hizo.

Amesema dawa pekee ya kutatua mgogoro huo ni mkuu wa mkoa Dodoma kufika katika eneo la tukio ili aweze kujionena na kupewa maelezo ya kina kwani kwa sasa mkuu wa wilaya kongwa hawezi tena kwani amekuwa akiwatetea wafugaji.

Alipotafutwa mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deogratias Ndejembi hakuweza kupatikana, hata simu yake ya kiganjani haikupatikana.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!