Sunday , 3 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa TAKUKURU wamnasa Diallo
Habari za SiasaTangulizi

TAKUKURU wamnasa Diallo

Anthony Diallo, Mmiliki wa Sahara Media ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza,
Spread the love

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), imemtia mbaroni, Anthony Mwandu Diallo, ikimtuhumu kugawa mrungula katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Mwanza, anaandika Moses Mseti.

Taarifa kutoka Mwanza zinasema, Diallo alitiwa mbaroni leo Ijumaa, majira ya saba mchana wilayani Ukerewe, ambako inaelezwa kuwa alikwenda visiwani humo kugawa fedha ili kuwashawishi wajumbe wa mkutano mkuu mkoani humo, kumchagua kuwa mwenyekiti wao.

Uchaguzi mkuu wa CCM kwenye ngazi ya mikoa umepangwa kuanza kuanzia kesho Jumamosi; mkoani Mwanza uchaguzi huo umepangwa kufanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Mwanza, Ernest Makale amethibitisha kushikiliwa kwa Diallo na taasisi yake.

Amesema, “ndio tunamshikilia Anthony Diallo, kwa tuhuma za kutoa rushwa kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi. Tumefanya hivi,  baada ya kupata taarifa kuwa anagawa fedha kwa wapiga kura katika uchaguzi utakaofanyika kesho.”

Anasema, taasisi yake inaendelea kumhoji Diallo na  baada ya hapo hatua nyingine zitachukuliwa kwa mujibu wa kanuni, sheria na taratibu.

Diallo, anayegombea nafasi hiyo kwa mara ya pili, katika uchaguzi huu, anakabiliwa na kibarua kigumu cha kukabiliana na mpinzani wake wa karibu, aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Meck Sadick.

Sadick ambaye aliamua kustaafu nafasi yake ya mkuu wa mkoa kwa hiari, anaonekana kuungwa mkono na wajumbe wengi wa mkutano huo, jambo ambalo linadaiwa kumlazimisha Dialo, kuamua kutembeza fedha kutetea kiti chake.

Gazeti hili limeshindwa kumpata mwanasiasa huyo kujibu madai hayo. Mwandishi alipomtafuta kwa simu yake ya mkononi majira ya saa 15: 51 (leo), mara zote ilikuwa inaita bila kupokelewa.

Hata hivyo, mara kadhaa Diallo amekuwa akikana madai kuwa anatumia fedha kutafuta ushindi.

Amesema, tuhuma kuwa anatumia fedha kuhalalisha uenyekiti wake, zimekuwa zikitolewa na baadhi ya wapambe wa mshindani wake huyo.

Diallo ambaye amepata kuwa waziri katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete na mmiliki wa kituo cha televisheni cha Star TV na Radio Free Africa, amekuwa akiandamwa pia na tuhuma za kumchafua mgombea mwenzake.

Update: 12:15

Habari ambazo zimetufikia muda huu zinasema, tayari Diallo ameachiwa huru na TAKUKURU na anaendelea na kampeni zake ya kutetea nafasi yake wilayani Magu.

 

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

20 wafariki dunia kwa mafuriko Manyara

Spread the loveMVUA za vuli zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini zimeleta madhara...

Habari za Siasa

Dk. Biteko aagiza wakurugenzi TANESCO kukemea rushwa kwenye maeneo yao

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Uongozi wa Samia kuendelea hadi 2030

Spread the loveKWETU sisi tuliowahi kusoma sekondari, iwe O levo au A...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Bado askari wastaafu wanaonewa

Spread the loveRAIS wangu Samia Suluhu Hassan tunaendelea kumshukuru Mungu kwamba wote...

error: Content is protected !!