Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Watetezi haki za binadamu walaani kukamatwa wanaopinga mkataba DP World
Habari za SiasaTangulizi

Watetezi haki za binadamu walaani kukamatwa wanaopinga mkataba DP World

Spread the love

WADAU wa haki za binadamu nchini na mashirika ya kimataifa wamelaani kitendo cha kukamatwa kwa wanasiasa na wanaharakati wanaopinga mkataba ushirikiano wa kiuchimi na kijamii baina ya Tanzania na Dubai kupitia Kampuni ya DP World ambayo inatarajiwa kuwekeza katika bandari za Tanzania.

Pia wameitaka Serikali kuwaachia watu hao waliokamatawa akiwamo mwanasiasa mkogwe nchini, Dk Wilbroad Slaa bila masharti yoyote.  Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hayo yanajiri ikiwa ni siku chache baada ya polisi kumshikilia Mwanadiplomasia huyo, jumapili ya tarehe 13 Agosti 2023, akiwa katika mjadala wa kisiasa uliokuwa ukirushwa moja kwa moja kupitia mtandao wa kijamii wa Club House.

Akisoma taarifa hiyo ya pamoja ya wadau ha oleo tarehe 15 Agosti 2023, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Anna Henga amedai mbali na Dk. Slaa wengine waliokamatwa ni Peter Madeleke, Boniphace Mwabukusi na Mdude Nyagali.

Wadau hao walioungana kwa pamoja ni Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu (LHRC) pamoja na Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS).

“Kama ilivyofanyika kwa Wakili Boniface Mwabukusi na Nyagali, Dk Slaa alihojiwa kwa tuhuma za uchochezi lakini baadae tuhuma zikabadilishwa na kuhojiwa tena kwa tuhuma za uhaini,” amesema Henga.

Akisoma tamko hilo, Henga ametoa wito kumtaka Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuingilia kati suala hilo ili watuhumiwa waachiwe bila masharti kwani ni dhahiri kwamba hawajatenda kosa la uhaini hata kidogo kulingana na masharti ya kosa hilo.

Pia wamelitaka Jeshi la Polisi kuheshimu haki na uhuru wa kutoa maoni huku wakisisitiza mapendekezo ya Tume ya Jaji Chande kuhusu mfumo wa haki jinai nchini yaheshimiwe.

Pamoja na watetezi wa kutoka nchini, pia Shirika la utetezi wa haki za binadamu la kimataifa, Amnesty International limetoa taarifa leo na kuzitaka mamlaka za nchini kuwaachia mara moja bila masharti.

Kamata kamata hii ilianzia kwa Wakili Boniface Mwabukusi na Mwanaharakati wa kisiasa, Mdude Nyagali ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kukosoa mkataba wa bandari ya Tanzania na kampuni ya DP World ya Dubai.

Hivi karibuni Mkuu wa Majeshi nchini IGP Camilius Wambura aliwaonya wale aliowataja kuwa wanapanga njama ya kumpindua Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!