Saturday , 30 September 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Wanafunzi 800 watumia madarasa 4
Elimu

Wanafunzi 800 watumia madarasa 4

Spread the love

KUKOSEKANA kwa vyumba vya kutosha vya madarasa katika shule ya msingi ya Mamboya iliyopo Kijiji na kata ya Mamboya Tarafa ya Magole Wilayani Kilosa mkoani Morogoro kumesababisha wanafunzi waliostahili kukaa madarasa mawili kusomea ndani ya darasa moja wakati wa masomo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea)

Wakizungumza na waandishi wa habari wanakijiji wa Kijiji hicho akiwemo Chiduo Chadibwa alisema shule hiyo ina madarasa manne pekee na wanafunzi 800 jambo linalosababisha wanafunzi kukaa zaidi ya 45 darasani kama inavyotakiwa kulingana na sera ya elimu.

“Wanafunzi wanakaa bila kufuata miongozo wala sera ya elimu darasani, darasa moja hukaa wanafunzi wa madarasa mawili mfano wa darasa la tatu na la nne, sasa hapo ni sahihi kweli nah ii ni haki elimu… sababu kila mtoto anasoma masomo ya darasa lake,” alisema Chadibwa.

Alisema awali kuliwa na madarasa yote yaani la kwanza hadi la saba lakini madarasa mengine mawili darasa la sita na la saba yalisemekana kuwa ni mabovu na kuvunjwa ambapo mpaka sasa mabati yake zaidi ya mia moja hayaeleweki yalipopelekwa.

Alisema kama wananchi walioguswa na changamoto hiyo kwa wanafunzi, na kufyatua matofali zaidi ya 3000 lakini mpaka sasa bado hawajapata mwongozo wowote kutoka kwa viongozi ili waanze ujenzi wa madarasa kukabiliana na changamoto hiyo.

Naye Mwamvita Mgulu mkazi wa Mamboya alisema shule hiyo pia inakabiliwa na changamoto ya uchache wa nyumba za kuishi walimu na kusababisha baadhi ya walimu kuishi kwenye vijiji vya mbali na shule na na kuwepo kwa changamoto ya ufundishaji kwa wanafunzi hasa nyakati za masika.

Mgulu alisema licha ya kuwepo kwa walimu 8 mmoja akiwa ni wa kike lakini kuna nyumba mbili tu za walimu ambazo haziwatoshi walimu wote.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Kisena Mabuba alisema tayari Halmashauri imeliona hilo na kupanga kuanza ujenzi wa madarasa matatu mwaka huu kupitia bajeti ya mwaka wa fedha 2013/14.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Elimu

Viwanda zaidi ya 200 kuonyesha bidhaa maonyesho ya TIMEXPO Dar

Spread the loveSHIRIKISHO la Wenye Viwanda Nchini (CTI) kwa kushirikiana na Mamlaka...

Elimu

Wazazi wa wanafunzi waliokosa nafasi vyuo vikuu waonyeshwa njia na GEL

Spread the loveWAKALA wa Elimu ya Vyuo Vikuu Nje ya Nchi, Global Education...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

Elimu

Green Acres kuwakatia bima wanafunzi wote

Spread the loveShule ya Green Acres imejipanga kufanya mambo makubwa kwa mwaka...

error: Content is protected !!