Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NIC yatunukiwa cheti cha Superbrand kwa mafanikio sekta ya bima
Habari Mchanganyiko

NIC yatunukiwa cheti cha Superbrand kwa mafanikio sekta ya bima

Spread the love

 

KATIKA jitihada za kutambua ufanis na utoaji wa huduma bora katika sekta ya bima nchini, Shirika la Bima la Taifa, NIC, imepokea cheti cha ubora kutoka kwa taasisi ya Superbrands kuwa kinara katika sekta hiyo ikiwa ni baada ya kufanyika kwa utafiti na tathmini ya kina ya huduma zake. Heshima ya kipekee ni uthibitisho kujizatiti imara kwa NIC katika weledi, ubunifu, na utoaji wa bidhaa na huduma za bima za ubora wa hali ya juu kuwahudumia Watanzania nchini kote. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).           

Kutambuliwa kwa NIC na Superbrand kunaonesha namna kampuni ilivyojikita katika kuboresha viwangu vya juu vya ubora, kuwajali wateja, na kuzingatia weledi. Tukio hili si mafanikio tu kwa NIC, bali inaonyesha jitihada za makusudi na mchango wa pamoja unaonyeshwa na wafanyakazi, washirika, na wadau wote.

Shirika la bima la Taifa, NIC, kwa muda mrefu linajiendesha kama kinara katika soko la huduma za hisa nchini, likihudumia mahitaji ya wateja kwa kuwapatia huduma tofauti za bima ambazo zinalinda Maisha, mali, na biashara zao. Cheti hiki cha kutambuliwa na Superbrands, kinaiweka NIC kwenye nafasi ya kuwa shirika linaloaminiwa na mtoaji wa huduma endelevu za bima, na kuonyesha kujizatiti kwakwe kuhakikisha usalama katika masuala ya kifedha na kuwapatia utulivu wa akili kwa wateja wake.

Mkurugenzi Mtendaji wa NIC, Dk. Elirehema Doriye ameonyesha furaha yake kwa mafanikio ya kutambuliwa na cheti hiki cha heshima kwa kusema kuwa, “ni heshima kubwa kupokea cheti cha utambulisho kutoka kwa taasisi ya Superbrand. Kutambuliwa huku ni uthibitisho wa kazi kubwa tunayoifanya Pamoja na kujitolea kwa kila mfanyakazi wa NIC, na inatuongezea chachu zaidi ya kuendelea kuboresha viwango vya huduma katika ya bima Tanzania.”

Kujitolea kwa NIC katika shughuli zake kwa kuzingatia weledi ni wa namna ya kipekee. Shirika limejizatiti kuendelea kuleta maendeleo chanya kwa jamii na kuchangia kwenye shughuli za kijamii na kiuchumi kwa maendeleo ya Tanzania. Kutambuliwa na Superbrand kumekuja wakati sahihi na kuongeza ari zaid ya NIC kuendeleza ubora wa viwango vya hali ya juu, kutumia ubunifu na teknolojia ili kuwapatia wateja huduma wanazohitaji na kusaidia sekta nzima kusonga mbele zaidi.

Mkurugenzi Mtendaji wa NIC, Dk. Elirehema Doriye

Wakati NIC ikisonga mbele, pia inaipokea heshima ya cheti hiki cha ubora kama changamoto ya kuwa bora zaidi na kuendelea kutoa huduma za kipekee, kuborasha ubunifu, na kuchangia maendelea chanya kwa ukuaji na ustawi wa Tanzania.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

error: Content is protected !!