Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Watanzania sasa kutuma na kupokea Pesa nchi za SADC
Habari Mchanganyiko

Watanzania sasa kutuma na kupokea Pesa nchi za SADC

Dk. Stargomena Tax, Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Spread the love

 

KAMPUNI ya simu za Mkononi ya Vodacom imezindua huduma  ya Vodacom M-Pesa inayoitwa “Dunia Kijiji, Afrika ni M-Pesa” ambayo inawawezesha Watanzania kutuma na kupokea pesa katika nchi za Ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Huduma hiyo ilimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam ambapo ukiacha nchi za Afrika Mashariki imepanua Huduma yake wa Fedha wa Kimataifa (IMT) moaka katika nchi za Afrika Kusini, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Lesotho, Msumbiji, Swaziland na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Dk. Stargomena Tax, Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo alisema, hatua hiyo ni kubwa katika maendeleo ya uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Waziri huyo ambaye aliwahi kuhudumu katika Jumuiya ya SADC, alisema Watanzania wanatakiwa kutambua kuwa huduma hii ni muhimu na waitumie vizuri kujikwamua kiuchumi katika ukanda huo wa SADC.

“Nikiwa SADC tulianzisha huduma ya Fedha Jumuishi kwa nchi hizo, hivyo kilichofanywa na M-Pesa ni sehemu ya ule mpango. Wamenigusa moyo wangu.

“Mbali na ukuaji wa kiuchumi, lakini hatua hii imesaidia mtu mmoja mmoja kwani inarahisisha gharama za kutuma pesa na urahisi kwani hii pesa zinamfikia mlengwa kwa wakati huo huo ambao anadhamiria kutuma,” alisema Waziri Tax.

Dk. Stargomena Tax, Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (katikati)

Waziri Tax pia aliipongeza Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ambaye ndiyo mdhibiti wa pesa za kimataifa kwa kufanya kazi na makampuni ya simu ili kuhakikisha kuwa malipo ya kimataifa yanakuwa salama.

“Naipongeza BoT kwa kutoa leseni kwa Vodacom chini ya kifungu cha16 (3) ya kanuni ya ubadilishaji wa nje ya 2022 ambayo inaruhusu Watanzania na M-Pesa kutuma pesa zaidi ya Afrika Mashariki na sasa kwa nchi za SADC,” alisema Waziri Tax.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa M-Pesa Tanzania, Epimack Mbeteni alisema M-Pesa baada ya kufanya vizuri katika ukanda wa Afrika Mashariki sasa wameamua kupanua wigo huo kwa nchi za SADC.

Mbeteni amesema safari ya Vodacom M-Pesa IMT ilianza mnamo 2014 kwa kuungana na Kenya, ambapo mnamo 2019 wakifanikiwa kupanya wigo na kuanza kutuma na kupokea pesa kwa nchi zote za Afrika Mashariki huku wakiwa wanapokea pesa kutoka nchi zaidi ya 200 duniani.

Mkurugenzi wa M-Pesa Tanzania, Epimack Mbeteni

Alisema mnamo Septemba 2021, waliongeza kipengee kipya ambacho kinawawezesha wateja wa Tanzania kutuma malipo kutoka M-Pesa kwenda kwa akaunti zote za Benki nchini Kenya, Uganda, na Rwanda.

Alisema malipo ya kimataifa yanekuwa msaada kwa watu binafsi na wafanyabiashara ndogo ndogo ambao kwa sasa wamekuwa wakifanya miamala bila kujali jiografia.

“Mbali na masuala ya biashara lakini pia mfumo huo umerahisisha kwa wanafunzi wanaosoma nje ya nchi, wagonjwa wanaotibiwa lakini pia hata ndugu na jamaa ambao wanaweza kutumiwa pesa na kupokea,” alisema Mbeteni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NEMC yatoa elimu matumizi sahihi ya zebaki kwa wachimbaji

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Oryx gesi yagawa mitungi, majiko 100 kwa waandishi wa habari Dar

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gesi Tanzania imegawa mitungi 100 ya gesi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari MchanganyikoMichezo

Wanamichezo Mei Mosi wachangia wahitaji vitu vya mil. 11.5

Spread the loveWanamichezo wanaoshiriki Michezo ya Mei Mosi Taifa 2024 jijini Arusha...

error: Content is protected !!