April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wapinzani kujitoa uchaguzi serikali za mitaa, kwaitesa CCM

Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM

Spread the love

HATUA ya vyama nane vya upinzani kujitoa katika kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2019, ilishtua Chama cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 18 Januari 2020 na Humphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, wakati akizungumza katika darasa la itikadi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, jijini Dar es Salaam.

Polepole amesema CCM ilipata mshtuko kwa kuwa, haikutegemea kama vyama hivyo vya upinzani vingechukua hatua hiyo.

Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi CCM amesema, chama chake kilijipanga kufanya kampeni kwa ajili ya kuchuana katika uchaguzi huo.

“Walipojitoa tumebaki CCM, tulikuwa tunawasubiri, tumejipanga kupiga kampeni hatari lakini wamejitoa wote. Tumepata mshutuko sababu nilikuwa najua nitapiga hapa, nitapiga kule lakini hakuna,” ameeleza Polepole.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ACT-Wazalendo, Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), ni miongoni mwa vyama nane vilivyosusia uchaguzi huo uliofanyika tarehe 24 Novemba 2019, kwa maelezo kwamba mchakato wake ulikuwa unapendelea wagombea wa CCM.

Katika uchaguzi huo, CCM ilishinda kwa asilimia 99.9 baada ya wagombea wake katika nafasi za uenyekiti wa kijiji, serikali za mitaa na kitongoji kupita bila kupingwa.

error: Content is protected !!