October 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Bashiru amtumia ujumbe Zitto Kabwe

Dk. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Spread the love

DAKTARI Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ametuma salamu kwa Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini, kwamba ajiandae kuliachia jimbo hilo, katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Bashiru ametoa salamu hiyo leo tarehe 18 Januari 2020, katika ziara yake mkoani Kigoma.

Mtendaji huyo wa CCM amesema ziara yake mkoani humo, imelenga kufunga mitambo ya ushindi katika uchaguzi mkuu wa wabunge na madiwani, huku akisisitiza kwamba chama chake kitachukua majimbo na halmashauri zote,  zilizochukuliwa na wapinzani.

“Nimekuja kutoa ujumbe Kigoma nzima na kule ambako bado tulishindwa, ikiwemo Kigoma Mjini kwamba tumejipanga kushinda. Na kwa hiyo wajiandae kukubali kushindwa wakati ukifika, nimekuja kufunga mitambo,” amesema Dk. Bashiru.

Wakati huo huo, Dk. Bashiru amevitaka vyama vya upinzani kukubali matokeo, pindi vitakaposhindwa katika uchaguzi huo.

“WanaCCM tukishindwa tukubali tumeshindwa na mara nyingi tukishindwa hukubali kwamba tumeshindwa,” amesema Dk. Bashiru na kuongeza.

“Tuliposhindwa Kigoma Mjini ubunge na halmashauri tulikubali. Na wao wajifunze pia kwamba, unaposhinda uliyemshinda akikubali ujue ipo siku akirudi raundi ya pili, akikung’oa nawe ukubali.”

error: Content is protected !!