Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Wanawake Afrika wampa tuzo ya heshima Balozi Mongela
Habari za Siasa

Wanawake Afrika wampa tuzo ya heshima Balozi Mongela

Spread the love

Wito umetolewa kwa wanawake kujiamini na kujipambanua kitaifa na kimataifa kwenye kusimamia ajenda za maendeleo yenye usawa wa kijinsia na kupinga ukatili wa kijinsia na kwa watoto. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dk. Dorothy Gwajima ametoa wito huo wakati wa hafla ya kumkabidhi, Balozi Dk. Getrude Mongella tuzo ya heshima, iliyofanyika jijini Dar Es Salaam Novemba 18, 2023.

Tuzo hiyo iliyotolewa na Umoja wa Wanawake wa nchi Huru za Afrika (PAWO-Africa) tarehe 31 Julai 2022 nchini Namibia, lengo lake ni kutambua mchango wa Balozi Getrude kwenye uongozi wa ngazi mbalimbali za Kimataifa ikiwemo kuwa rais wa utetezi wa wanawake Afrika na rais wa kwanza wa Bunge la Afrika.

Vilevile, Balozi Getrude amekuwa Mshauri Mwandamizi na Katibu Mtendaji wa Kamisheni Uchumi ya Afrika katika masuala ya Jinsia, Mlezi wa Asasi za Kiraia zisizo za Kiserikali pamoja na kusimamia Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya Wanawake Jijini Beijing nchini China Septemba, 1995.

Dk. Gwajima amempongeza Balozi Getrude kwa ujasiri na uthubutu wake kwenye kutoa mchango wake kwa maendeleo ya wanawake na kuhimiza kuwa, mafanikio haya yakawe chachu kwa Wanawake wengine wote kujiamini kusimamia ajenda za maendeleo ya wanawake.

Aidha, Dk. Gwajima amewahakikishia Wanawake kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan tayari ameweka mazingira mazuri kwa Wanawake wote wenye mchango kwenye safari ya maendeleo yenye usawa wa kijinsia kuendelea kusimama kwenye nafasi zao ikiwemo, kwenye kutokomeza ukatili wa kijinsia na kwa watoto.

Kwa upande wake Balozi Getrude ameshukuru kwa kutambuliwa kwake ambapo amesema, utambuzi huo ni kwa ajili ya wanawake wote walioshiriki kupigania haki za wanawake tangu kuundwa kwa PAWO mwaka 1965.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawale Tanzania (CWT) Mary Chatanda amempongeza Balozi Getrude na kutoa wito kwa Wanawake wote kuunganisha nguvu na kuelekeza juhudi zao kwenye kupambana kutokomeza ukatili wa kijinsia na kwa Watoto.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

Habari za SiasaTangulizi

Maafa Manyara: Rais Samia akatisha ziara yake Dubai

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekatisha ziara yake...

Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the loveWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na...

error: Content is protected !!