Sunday , 3 December 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Wanawake 104 waliodaiwa kubakwa walipwa 624,000 kila mmoja
KimataifaTangulizi

Wanawake 104 waliodaiwa kubakwa walipwa 624,000 kila mmoja

Spread the love

Shirika la afya duniani WHO limewalipa limewalipa  fidia ya Dola 250 (Sh 624.3) wanawake 104 waathiriwa wa dhulma za kingono nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Kwa mujibu wa ripoti kutoka WHO, Dk. Gaya Gamhewage kutoka kitengo cha kupambana na dhulma za kingono katika shirika hilo, alisafiri kwenda DRC mwezi Machi  kulishughulikia suala hilo ambapo wafanyakazi wa WHO waliokuwa wakisaidia kupambana na mlipuko wa Ebola wanatuhumiwa kuwanyanyasa kimapenzi wanawake hao 104.

Dk. Gaya katika ripoti yake kwa UN kuhusu ziara yake, amesema alikutana na wanawake hao, mmoja wao akiwa amejifungua mtoto aliyekuwa na matatizo ya kiafya na kuhitaji kugharamika zaidi kupata matibabu maalum.

Wadadisi wamehoji kiasi hicho kilicholipwa na WHO kilikuwa kidogo ikilinganishwa na gharama ya safari ya Dk. Gaya ya siku tatu.

WHO kabla kufanya malipo hayo iliwasajili wanawake hao katika mafunzo ya kujifunza namna ya kujishughulisha na kupata kipato ingawa wengi wa akina mama waliodhalilishwa kimapenzi waliachwa nje WHO ikisema wengi wao walikataa ofa hiyo, huku asilimia kubwa wakiwa hawajulikani waliko.

Sakata hilo la dhulma za kimapenzi ambapo wafanyakazi 83 wa WHO wanatuhumiwa kuwabaka wanawake kati ya mwaka 2018 na 2021 wakati wa Ebola,ni sakata kubwa kuwahi kuandama WHO.

1 Comment

  • Haibu sana kwa UN institutions !!!….. 250 USD ?? Kwa kila aliye tajwa kubakwa na wafanya kazi wa WHO waliokuwepo kipindi Cha corona !; who will be responsible for the future life of those wonderful congolese young girls that you stopped their future life ??;…. To be continued; Life is a long way learning! Siku moja those oppressed girls will enjoy your end !!!….. 250 USD , I can’t even start a single hour of life’s living with that small amount of money. 🙏🙏

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

20 wafariki dunia kwa mafuriko Manyara

Spread the loveMVUA za vuli zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini zimeleta madhara...

Kimataifa

Muandamanaji ajichoma moto akipinga vita Palestina, Israel

Spread the loveMUANDAMANAJI moja ambaye hajafahamika jina, yuko mahututi hospitalini akitetea uhai...

Kimataifa

Urusi kuongeza wanajeshi ikijihami dhidi ya NATO

Spread the loveSERIKALI ya Urusi iko katika mpango wa kuongeza wanajeshi wake,...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu aanika matobo miswada sheria za uchaguzi

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu...

error: Content is protected !!