March 4, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wanaofelisha watoto wapewa somo

Mtoto akichunga

Spread the love

WAZAZI na walezi wilayani Bahi mkoani Dodoma wametakiwa kuwekeza elimu kwa watoto wao wanaohitimu shule ya msingi na sekondari, kwa kuwaendeleza kimasomo zaidi badala ya kuwafanya warithi wa mifugo, anaandika Dany Tibason.

Pia amewataka wakulima wa wilaya hiyo kuaandaa mashamba yao kwa kuweka mbolea ili kukabiliana na mvua zinazotarajia kunyesha wakati wowote kwa mujibu wa watabiri wa hali ya hewa kwa mikoa ya kanda ya kati.

Ushauri huo umetolewa na Suleiman Yusuph, Shekhe wa wilaya ya Bahi alipokuwa akitoa mawaidha katika sala ya ljumaa iliyofanyika kwenye msikiti wa Kigwe wilayani humo.

“Wapo wazazi ambao wamekuwa wakiwataka watoto wao wafanye vibaya katika masomo yao au kuwazuia wasiende shule ili waweze kuwa wasimamizi wa mifugo, kurithi mashamba.

“Kwa ulimwengu tulionao uwezi kuwekeza kwa kumpatia mtoto elimu mifugo, jambo pekee ambalo mtoto anaweza kujivunia ni pale ambapo utaweza kumpatia elimu bora na si bora elimu” amesema Sheikh Yusuphu.

Amesema kuwa hakuna sababu ya kutowaendeleza watoto hao wanaomaliza elimu hiyo wakati serikali ya awamu ya tano imeshaomdoa michango mbalimbali ambayo ilikuwa kikwanzo katika kumwendeleza mtoto shule.

“Serikali ya awamu ya tano  michango imeondolewa ikiwemo ada kwa kuzifuta kuanzia shule za msingi hadi kidato cha nne,hivyo sioni sababu ya kumkwamisha mtoto kielimu hapa”alisema.

Akizungumza kuhusu kilimo aliwataka wakulima kuhakikisha wanaandaa mashamba hao kwa kuweka mbolea ikiwa na pamoja na kupanda mazao yanayolingana na hali ya mvua zinazonyesha kwa mikoa hiyo.

Awali akizungumza na waumini wa msikiti huo kwa upande wao aliwataka kufuata miongozo ya dini ya kiislamu siku zote za maisha yao ikiwemo kudumisha amani,upendo,umoja na mshikamano.

error: Content is protected !!