Saturday , 13 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Waliombeza Dk. Shika kuumbuka, adai mabilioni yake kutua Tanzania
Habari za SiasaTangulizi

Waliombeza Dk. Shika kuumbuka, adai mabilioni yake kutua Tanzania

Dk. Louis Shika
Spread the love

BILIONEA wa nyumba za Lugumi aliyeteka vichwa vya habari siku za hivi karibuni, Dk. Louis Shika, amekamilisha malipo ya bima kwa ajili ya kutumiwa fedha zake kutoka nchini Urusi, anaandika Nasra Abdallah.

Dk. Shika aliingia matatani baada ya kushinda mnada wa uuzwaji wa nyumba za Said Lugumi hali iliyosababisha kukamatwa na polisi, lakini binafsi alisisitiza kuwa fedha hizo anazo na sasa anaelekea kuthibitisha hilo kwa kufanya mchakato wa kutumiwa fedha. 

Waandishi wa habari walimkuta Dk. Shika akiwa katika huduma za mtandao wa internet katika shirika la Posta Jijini Dar es Salaam, ambao walikuwa katika ziara ya Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Atashasta Nditiye na kujikuta hata mwenyewe akimshangaa bilionea huyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kutuma taarifa za miamala hiyo, Dk. Shika amesema ametuma kiasi cha dola 100 ambapo anatarajia muda si mrefu ataweza kutumiwa fedha zake na kwenda kulipia asilimia 25 ya fedha zinazotakiwa katika nyumba hizo.

Alipoulizwa kama fedha hizo zikichelewa na kukuta mchakato huo wa malipo umepita, amesema kwa kujiamini, atanunua nyingine kwani Dar es Salaam kuna nyumba nyingi zinazouzwa siyo lazima hizo za Lugumi.

Kiasi hicho cha fedha, amekilipa kwa kwa Benki ya Equity kwenda Benki ya Bankok nchini Thailand, mchakato utakaomwezesha kutumiwa fedha zake na kuweza kununua nyumba hizo.

Katika hatua nyingine Dk. Shika alisifia huduma za shirika hilo na kueleza kwamba ndiyo hutuma huduma za internet katika kutuma nyaraka zake mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Nchimbi aanika ugonjwa wa CCM

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Emanuel Nchimbi,...

Habari za Siasa

Chadema yapuliza kipyenga uchaguzi viongozi kanda

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeanza maandalizi ya uchaguzi...

Habari za Siasa

CCM :Hatutaki ushindi wa makandokando uchaguzi Serikali za mitaa

Spread the loveCHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakihitaji ushindi wa makandokando katika...

Habari za Siasa

Makala: Puuzeni wanasiasa wanaojigamba wanaweza kubadili maamuzi ya mahakama

Spread the loveKATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),...

error: Content is protected !!